RC Makonda: Baada ya kumuumbua Mbowe nimewaokoa wananchi wa Dar es Salaam

Elitwege

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
5,154
10,809
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam leo amejibu tuhumu za kukosolewa na waziri wa afya kufuatia kitendo chake cha kumtaja mgonjwa wa Corona ambae ni mtoto wa Mbowe.

Paul Makonda amesema kabla ya kumtaja mtoto wa Mbowe mwenye Corona alikuwa anatibiwa nyumbani na hakutengwa karantini kama taratibu zinavyotaka.

Mara baada ya Mbowe kuumbuliwa kwamba Corona ipo kwenye familia yake ndiyo akaamua kumpeleka hospital mtoto na yeye mwenyewe Mbowe kuamua kujiweka karantine na familia yake huko Dodoma.

Makonda amesema kama asingemtaja mtoto wa Mbowe basi huyo mtoto angeendelea kutibiwa nyumbani na Mbowe angeendelea kuzunguka na kufanya press conference pamoja na kuhudhuria vikao bungeni.

Kwa hiyo Paul Makonda amewaokoa wananchi wa Dares salaam na wa Tanzania Kwa ujumla hivyo asilaumiwe.


====



















Source: Ayo Tv

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbe kuna ambao wanaopelekwa ma-hosipalini kwa matibabu na kuna ambao wanaolazimishwa kwenda mahotelini ya gharama na kutelekezwa huko...



Cc: mahondaw
 
Mimi nashangaa watu wanaomshangaa Bashite. Binafsi nilliisha acha kumshangaa zamani sana kwa kuwa najua kichwani ni zero kwa hiyo. Kwa hiyo kila tamko analotoa ndio kikomo chake cha kufikiri. Poleni sana wana DSM kwa kuwa na kiongozi bomu kama huyo!
 
Back
Top Bottom