RC Makonda ataka Spika Ndugai aanze utaratibu wa kupima wabunge kugundua watumiaji wa madawa

Naye wakampime ustaarabu wa nyuma sababu inasemekana Marinda wametatua By SUGU moto chini
 
Baadhi ya Wabunge walipomtuhumu Makonda walikuasahii!! ila Makonda anapomkumbushia Spika kuhusu kauliyake yakuwekavifaa vya kuwapimaWabumge kama wanatumia madawayakulevya anakosea!!
Sasa napata picha kwanini Makonda sikuzote anafanikiwa kwenye kazizake. nikwakua sikuzote anasemaukweli. Mungu sikuzote anasimama upande wa haki. Uwezi leo umwitemtu fisadi alafu kesho usimame mbeleya umma wa Mwenyezi Mungu ukimsafisha kinafiki yule uliyemtuhumu.
Munguwahaki apendi mizaha, mwangalie Lema kaulizake zinavyomtesa, jamani Mungu hataniwi.
Kipi alichofanikiwa Makonda katika mkoa wa DSM? Mana panda mti imekufa kifo cha mende,oparesheni ondoa ombaomba hamna kitu,shisha na mashoga vimeshamili kwa Dar
 
Hii Makonda atakuwa amewadharau wote walio mle Bungeni. Kwani kama unataka kupima wabunge basi unamaanisha wote waliopo mule lazima wapimwe. Spika na naibu wake lazima wapimwe, Majaliwa kama Mbunge atapimwa, Ag na mawaziri wote lazima wapimwe kwani huwezi kubagua.
Hilo ni utovu wa nidhamu wa Makonda kwa mabosi wake yaani PM na mawaziri. Amewadharau labda kwa vile ana urafiki na mteuzi mwenyewe.
Dogo anafika mbali sana hii nguvu anaitoa pale MAGOGONI...
 
Makonda amegeuka kuwa spika sasa! Makonda hukuchaguliwa na wananchi uliteuliwa na Mkuu. Ukuu wa mkoa wa Dar sio ukuu wa nchi au mikoa yote ya Tz.
 
Mimi ningependekeza tuwapime kwanza polisi mikojo yao tuone kama kuna chembechembe za madawa!
 
Hii Makonda atakuwa amewadharau wote walio mle Bungeni. Kwani kama unataka kupima wabunge basi unamaanisha wote waliopo mule lazima wapimwe. Spika na naibu wake lazima wapimwe, Majaliwa kama Mbunge atapimwa, Ag na mawaziri wote lazima wapimwe kwani huwezi kubagua.
Hilo ni utovu wa nidhamu wa Makonda kwa mabosi wake yaani PM na mawaziri. Amewadharau labda kwa vile ana urafiki na mteuzi mwenyewe.
Nini wewe mtumia ngada, yaani kwa vile mtu amekuwa mbunge ndio awe juu ya sheria ? M/kiti wenu amewaharibu kwa madawa nyie ufipa camp, sasa naanza kuamini yani huwezi kuwa mzima wewe poda limekuharibu ubongo. Ata Rais kama vipi apimwe tu wachia mbali PM. Lengo ni kuwa na viongozi wasafi wasokula wala kuuza hutaki hama nchi.
 
RC Makonda amemkumbusha Spika wa Bunge kuhusu kuweka vyombo vya kuwapima nani anatumia au alikwisha kutumia madawa ya kulevya.

Naamini hilo mtalipinga kwa nguvu zenu zote na kumtaka RC Makonda ajieleze kwenu, ati kwa kuwadharau. Lakini tunawaamini kuwa mtakuwa kitu kimoja kukubali kupimwa ili kulinda heshima yenu na ya Bunge.

Makonda kwa nafasi yake hana mamlaka ya kumuagiza spika wa bunge hata siku moja , hata kama wewe ni mfuasi wa makonda wakati mwingine unajaribu kufikiri kidogo.
 
Dharau ipi waihusisha na Makonda wakati alikuwa anarejea wazo la Spika kuweka kipimo kwa Wabunge wake!

Sishangai baadhi yetu humu jamvini kupinga Wabunge kutokupimwa matumizi ya unga, wakati ndo watunga sheria na wasimamizi wa utendaji wa Serikali.

Wakiwa mashujaa, kujiamini na kuonesha uadilifu wao, wakubali pia kupimwa magonjwa mengine ambukizi kama UKIMWI.
Hakuna anye pinga hilo ila kinacho pingwa ni makonda kujivika utukufu na ukuu hadi kwa mabosi wake na mihimili mikubwa kuliko mamlaka yake bila kujijua.
 
Mkuu mwengeso, kama ni suala la kuonyesha uadilifu huyo anayetaja wengine na kuwataka wabunge au viongozi wengine wapimwe ilifaa yeye awe wa kwanza kwenda kupimwa.

Maana kuongoza ni kuonyesha njia, hivyo yeye angeanza kuonyesha usafi wake hapo ndipo angekuwa na sifa ya kunyooshea wengine vidole.
 
Dharau ipi waihusisha na Makonda wakati alikuwa anarejea wazo la Spika kuweka kipimo kwa Wabunge wake!

Sishangai baadhi yetu humu jamvini kupinga Wabunge kutokupimwa matumizi ya unga, wakati ndo watunga sheria na wasimamizi wa utendaji wa Serikali.

Wakiwa mashujaa, kujiamini na kuonesha uadilifu wao, wakubali pia kupimwa magonjwa mengine ambukizi kama UKIMWI.
 
Hivi waingizaji na watumiaji ni Nani anayestahili kukamatwa? Mtaani mateja wamejaa tuu kama kuwakamata ndo mtamaliza tatizo sidhani kama mtafanikiwa. Eti wabunge wapimwe!!! Hv unaweza kunilazimisha kupima kitu kwenye mwili wangu bila ridhaa yangu? Ni raha na burudani kuongoza watu wasio Tambua haki zao. Kila kitu ni ushabiki tuu
 
RC Makonda amemkumbusha Spika wa Bunge kuhusu kuweka vyombo vya kuwapima nani anatumia au alikwisha kutumia madawa ya kulevya.

Naamini hilo mtalipinga kwa nguvu zenu zote na kumtaka RC Makonda ajieleze kwenu, ati kwa kuwadharau. Lakini tunawaamini kuwa mtakuwa kitu kimoja kukubali kupimwa ili kulinda heshima yenu na ya Bunge.

Ningemshauri Mheshimiwa huko apaache Kamishna yupo atashughulika. Si vema kutoa nafasi ya wanaomkosoa, kumkosoa pasipo sababu. Ya hapa mkoani Dar wengi tulimwelewa. Ni ushauri tu!
 
Katika hotuba ya makonda sehemu mojawapo aliyokosea ni hapo. Moja yeye ni mkuu wa mkoa wa Dar hivyo alipaswa kujikita kwenye mikakati ya mkoa wake lakini amejisahau akajua yeye ni kamishana

Pili bunge ni mojawapo ya mihimili mikuu ya jamhuri kama alitaka kusema juu ya mihimili basi angesema na mahakama hata ofisi kuu watu wachunguzwe kwa kushambulia bunge peke yake kutamletea mgogoro.
Ngoja tuone nani zaidi kondakta au mmoja Wa wamiliki Wa bus kati ya wamiliki watatu
 
  • Thanks
Reactions: 999
Back
Top Bottom