RC Makonda ataka Spika Ndugai aanze utaratibu wa kupima wabunge kugundua watumiaji wa madawa

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
8,204
2,000

RC Makonda amemkumbusha Spika wa Bunge kuhusu kuweka vyombo vya kuwapima nani anatumia au alikwisha kutumia madawa ya kulevya.

Naamini hilo mtalipinga kwa nguvu zenu zote na kumtaka RC Makonda ajieleze kwenu, ati kwa kuwadharau. Lakini tunawaamini kuwa mtakuwa kitu kimoja kukubali kupimwa ili kulinda heshima yenu na ya Bunge.
 
Saguda47

JF-Expert Member
May 1, 2016
8,542
2,000
Naomba nioneze hapo, ikulu pia wale wafanyakazi pele ikulu wale wa mambo ya sirisiri na wale wakupigapiga wanaovaa kofia nyekundu tunaomba wapimwe... Vilevile kama mnavyoitaji wafanyiwe wabunge
You're totally out of the pool!!
 
Kichakoro

JF-Expert Member
Sep 10, 2008
2,536
2,000
Katika hotuba ya makonda sehemu mojawapo aliyokosea ni hapo. Moja yeye ni mkuu wa mkoa wa Dar hivyo alipaswa kujikita kwenye mikakati ya mkoa wake lakini amejisahau akajua yeye ni kamishana

Pili bunge ni mojawapo ya mihimili mikuu ya jamhuri kama alitaka kusema juu ya mihimili basi angesema na mahakama hata ofisi kuu watu wachunguzwe kwa kushambulia bunge peke yake kutamletea mgogoro.
 
Juma wa Juma

Senior Member
Jan 13, 2017
151
250
Katika hotuba ya makonda sehemu mojawapo aliyokosea ni hapo. Moja yeye ni mkuu wa mkoa wa Dar hivyo alipaswa kujikita kwenye mikakati ya mkoa wake lakini amejisahau akajua yeye ni kamishana

Pili bunge ni mojawapo ya mihimili mikuu ya jamhuri kama alitaka kusema juu ya mihimili basi angesema na mahakama hata ofisi kuu watu wachunguzwe kwa kushambulia bunge peke yake kutamletea mgogoro.
Mgogoro wa nn wao wawakilishi wetu na wanapinga madawa sasa wawe mfano juu ya hili
 
The Monk

Platinum Member
Oct 12, 2012
15,777
2,000
Nafikiri hili liwe ni takwa la kikatiba kwa kugombea nafasi yoyote kuanzia ile kubwa kabisa. Kama kweli hii vita ya madawa ya kulevya ni ya kila mtanzania, hatuwezi kuwa na kiongozi anaejihusha au kutumia haya madawa. Wapimwe tu maana hakuna namna.
 
Mlaleo

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
12,089
2,000
Naona Mhimili unaanza kuingilia Mhimili Mwingine... Nyie hamtujui Wabunge naona... Kama mmelewa sifa mtang'oka
 
Alisina

JF-Expert Member
Aug 9, 2016
3,741
2,000
Kwa hili Nahakika haliwezi kutokea na hapo ndio utaona hakuna cha Upinzani wala Tawala, Wote watakuwa kitu kimoja hahaha hawa wanasiasa wetu wanavituko sana!!

-Waliopo hatuwaki kabisa lakini Wanao taka tuwape Nchi hatuwaamini-
 
mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
8,204
2,000
Katika hotuba ya makonda sehemu mojawapo aliyokosea ni hapo. Moja yeye ni mkuu wa mkoa wa Dar hivyo alipaswa kujikita kwenye mikakati ya mkoa wake lakini amejisahau akajua yeye ni kamishana

Pili bunge ni mojawapo ya mihimili mikuu ya jamhuri kama alitaka kusema juu ya mihimili basi angesema na mahakama hata ofisi kuu watu wachunguzwe kwa kushambulia bunge peke yake kutamletea mgogoro.
Mkuki kwa nguruwe!
 
Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
36,780
2,000
Hii Makonda atakuwa amewadharau wote walio mle Bungeni. Kwani kama unataka kupima wabunge basi unamaanisha wote waliopo mule lazima wapimwe. Spika na naibu wake lazima wapimwe, Majaliwa kama Mbunge atapimwa, Ag na mawaziri wote lazima wapimwe kwani huwezi kubagua.
Hilo ni utovu wa nidhamu wa Makonda kwa mabosi wake yaani PM na mawaziri. Amewadharau labda kwa vile ana urafiki na mteuzi mwenyewe.
 
Dharau ipi waihusisha na Makonda wakati alikuwa anarejea wazo la Spika kuweka kipimo kwa Wabunge wake!

Sishangai baadhi yetu humu jamvini kupinga Wabunge kutokupimwa matumizi ya unga, wakati ndo watunga sheria na wasimamizi wa utendaji wa Serikali.

Wakiwa mashujaa, kujiamini na kuonesha uadilifu wao, wakubali pia kupimwa magonjwa mengine ambukizi kama UKIMWI.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom