RC Makonda aamuru nyumba 36 kubomolewa bonde la mto Msimbazi

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,787


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam leo amefanya ziara kwa wakazi wanaoishi kwenye bonde la mto Msimbazi ili kujionea athari mbalimbali zilizotokea kwenye mafuriko.

Mkuu wa mkoa amewashukia wakazi wanaoishi bonde hilo waliojenga nyumba na kuziba mto, ukuta ulioziba mto na kuamuru halmashauri kubomoa nyumba hizo 36 bila kulipa fidia kuanzia kesho.

IMG_4172.JPG


Hatuwezi kuhatarisha maisha ya wananchi halafu serikali ije kupata lawama badae.

Wanaoishi kwenye bonde la mto wapo kwenye makundi matatu ambayo ni...

> Wale ambao wameshalipwa fidia na kuamua kupangisha watu ila wao wameondoka.

> Kuna waliopewa maeneo Mabwepande na wakauza na kurudi.

> Kuna wale bado hawajapata fidia
 
Yule mjane aliyelilia kwa rais amewafunza watu ujasiri wa kuwavakaa viongozi. Naona mama Yohana Jonas naye anajaribu bahati yake.
 
Mambo ya vyeti hayahusiki hapa.

Haiwezekani sisi walipa kodi,tunapanga nyumba bei ghali,watu wamevamia jangwani ,wamefidiwa,wamepewa viwanja mabwe pande,alafu hawaondoki.

Tuungane mkono na mheshimiwa RC Makonda kuwaondoa hawa watu.
Na si nyumba hizo tu,zote hata uwanja wa Yanga
Mwendo kasi nao wamevamia jangwa BOMOA!!!!
 
Mambo ya vyeti hayahusiki hapa.

Haiwezekani sisi walipa kodi,tunapanga nyumba bei ghali,watu wamevamia jangwani ,wamefidiwa,wamepewa viwanja mabwe pande,alafu hawaondoki.

Tuungane mkono na mheshimiwa RC Makonda kuwaondoa hawa watu.
Na si nyumba hizo tu,zote hata uwanja wa Yanga
wakishaondolewa
piga kazi baba... huwezi ona wananchi wako wanahatarisha maisha yao wakati kuna maeneo salama ya kuishi....
Watu wahamie maeneo salama yasiyofikiwa na mafuriko, sawa kabisa ila kuongozwa na mkuu wa mkoa aliyelangua vyeti ni issue nyingine kubwa, hapo anajitapatapa tu
 
Back
Top Bottom