RC Kilimanjaro Anna Mghwira alaani wahuni walioshambulia msafara wa Tundu Lissu

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira ameshutumu vikali kitendo kilichofanywa na vijana wahuni wanaodaiwa kukodiwa na kuushambulia kwa mawe msafara wa mgombea Urais kupitia Chadema Tundu Lissu.

Mkuu huyo wa mkoa alitoa kauli hiyo wakati akimjibu Mkuu wa KKKT dayosisi ya Kaskazini Askofu Shoo aliyetaka serikali ya mkoa kudhibiti vitendo hivyo ili kulinda Amani ya nchi.

Akinukuliwa na gazeti la Nipashe la leo Anna Mghwira alisema vitendo vilivyofanywa si vya kistaarabu na atachukua hatua na kutoa taarifa siku chache zijazo.

Wananchi wamekuwa wakimtuhumu Mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya kufadhili vikundi hivyo vya wahuni kushambulia mikutano ya Chadema kutokana na kujiapiza hadharani kwamba atatumia mamlaka yake kuhakikisha Freeman Mbowe hatashinda Tena ubunge katika Jimbo Hilo.

=====
MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira, amezungumzia tukio la kushambuliwa kwa mawe wilayani Hai mkoani Kilimanajro kwa msafara wa mmoja wa wagombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, akisema hakukuwa na sababu na uhalali wowote wa kufanyika kwa kitendo hicho.

Mghwira alitoa kauli hiyo jana alipojibu hoja iliyotolewa na Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dk. Frederick Shoo, aliyezungumzia tukio hilo wakati wa Mkutano Mkuu wa 36 wa Dayosisi ya Kaskazini, akitaka jambo hilo kukemewa.

Licha ya pande hizo mbili kutotaja jina la mgombea huyo, Ijumaa iliyopita kulisambaa picha za video kwenye mitandao ya jamii zikionyesha watu wakitupiana mawe wakati msafara wa mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, ulipoingia wilayani Hai. Wakati anatoa salamu za serikali, Mghwira alisema:

"Na ni kweli juzi Ijumaa, ninakiri alipita hapa mgombea mmoja, na katika Jimbo letu la Hai vijana pale wakaanzisha vurugu. "Lakini, baadaye nilipata taarifa jioni niliporudi, kwa sababu nilikuwa Same, niliambiwa kwamba yuko Arusha, lakini alipofika Hai kulitokea tatizo ambalo vijana walianza kutupiana mawe kweli bila sababu.

“Hakukuwa na sababu yoyote, wala hakukuwa na uhalali wowote, lakini hilo nitalisemea mahali panapotakiwa. Ninaomba tu kanisa litambue kwamba tumeona hitilafu hiyo iliyojitokeza, tumeifanyia kazi na mimi nitaitolea maelezo hivi karibuni."

KAULI YA DK. SHOO
Katika hotuba yake wakati anafungua mkutano huo, Dk. Shoo alisema: “Kipekee nimesikitishwa sana na vitendo ambavyo vinafanywa na vijana wahuni wachache, na sijajua nani anayewaongoza kushambulia mikutano ya wale ambao wanapita kutafuta wadhamini.

“Jambo hili linafaa kukemewa kwa sababu huo ni mwanzo, ni jambo la hatari ambalo linaweza likaleta shida na kuvuruga amani. Kwa ajili hiyo, niwaombe sana kwa pamoja na kwa nia njema kabisa, tukemee vitendo vya namna hiyo.

"Tukumbuke kwamba amani ni tunda la haki na uonevu unapokithiri na haki kukanyagwa, amani inaweza ikatoweka. Na hili linaweza likawa jambo la kufumba na kufumbua.”

Kiongozi huyo wa kanisa pia alisisitiza kuwa Watanzania wanapaswa kujifunza kwa nchi jirani madhara ya vitendo vya aina hiyo hasa nyakati kama hizi za uchaguzi au baada ya uchaguzi. “Mungu atunusuru ili lisitokee kwetu na sisi tusiwe sehemu ya visababishi.

Ninawahimiza wakristo na watu wote, Watanzania wenzangu kushiriki kwa haki, kushiriki usawa, uwazi, amani na utulivu katika machakato wa kuwapata viongozi bora, ili tusije tukafika mahali tukalalamika na kujutia kwamba kumekuwa na viongozi waovu.

"Wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu, sikilizeni wagombea ili upate ufahamu kama ana sifa sahihi za kiongozi bora na kufanya uchaguzi sahihi siku ya uchaguzi. "Ni kweli huwa sisi viongozi wenu, viongozi wa dini hatupaswi kuwa washabiki wa chama fulani, lakini ni wajibu wetu kuwasaidia watu kupata ujuzi wa kweli kuhusu mtu anayefaa kuwa kiongozi," Dk. Shoo alisema.

Askofu huyo pia aliwataka viongozi wa kanisa hilo na waumini wake kushirikiana na serikali na vyombo vingine vyote vya kusimamia uchaguzi mkuu na watu wengine wote wenye mapenzi mema.

Alisema kuwa wao wanaendelea kusisitiza Watanzania wanao wajibu wa kuchagua watu wafaao kuongoza na wala siyo chama.
“Tuangalie sana watu waadilifu, watu wacha Mungu, wenye nia ya dhati ya kuwatumikia Watanzania. Sisi Dayosisi ya Kaskazini tunapenda kuwahimiza Watanzania kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi huu.

"Tunapenda kutoa rai kwa wana dayosisi na jamii kwa ujumla, kuzingatia maadili mema kama kigezo kikuu cha kuwachagua viongozi wetu.

"Tunawasihi sana wanasiasa, viongozi wenzangu wa dini zote na Watanzania kwa ujumla, tudumishe haki, tudumishe amani na utulivu, kwani hizi ni tunu za pekee katika maisha ya taifa letu. Mkumbuke kwamba tunu ya amani ikiharibika, shughuli za maisha na ibada hazitawezekana," alisema.


Nipashe
 
Huyo RC ameamua kuusimamia ukweli

Pongezi kwake, kwani ni nadra sana kwa utawala huu, kiongozi kuusema ukweli wa aina hiyo 👏 👏
Ukweli upi?

Kwani hawajui waliofanya vulugu?
Angeaza kumkamata ole sabaya na genge lake ndiyo tungejua kuwa ameamua kuchukua hatua
 
Huyu mama nadhani hajui kilichomuweka hapo, na hivi Lissu ni 'home boy' wake.

Usishangae hadi kufikia jioni tukaona taarifa ya Gerson Msigwa, bwana Meko akafanya ile kazi yake pekee ambayo ameonesha kuimudu kwa awamu yake yote.
 
Hengai Ole Sabaya ana akili za kuchungua Ng'ombe au Ndama tu hata kama kaelimika

Nampogeza Mama Mughwai damu nzito bhana anaweza kutupiwa angalao kamfupa na Raisi wa Jamhuri Raisi TunduLissu
 
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira ameshutumu vikali kitendo kilichofanywa na vijana wahuni wanaodaiwa kukodiwa na kuushambulia kwa mawe msafara wa mgombea Urais kupitia Chadema Tundu Lissu...
Watu wenye wito wa Mungu utawajua tu kwa matendo yao Mama namkubali sana huyo
 
Ukweli upi?

Kwani hawajui waliofanya vulugu?
Angeaza kumkamata ole sabaya na genge lake ndiyo tungejua kuwa ameamua kuchukua hatua
Duh! Hapa Mama Anna Mgwira amejilipua. Ndani ya siku 2 atakuwa si RC tena. Yule mhuni aliratibu vijana kutupa mawe ndo atakuwa RC! You can take this to the bank!
 
Huyo RC ameamua kuusimamia ukweli.

Pongezi kwake, kwani ni nadra sana kwa utawala huu, kiongozi kuusema ukweli wa aina hiyo 👏
Kitakachomsave asitumbuliwe labda kwa kuwa ni Mwanamke ..... Inaelekea awamu hii kazi za wanawake ziko safe kidogo!!
 
Bora auseme ukweli moyo wake ubaki na amani kuliko kusimamia matendo ya kishetani ili kujaza tumbo, mambo ya kuneemesha tumbo amuachie Sabaya.
Ni kweli lkn yametendeka mengi hakuyatolea matamko ..na wengine wameenda mbali na kusema au kwa kuwa Lissu Ni msingida mwenzake ndo maana kalaani
 
Anatuzuga tu huyo mama ..kwn lile Ni tukio la kwanza?
Alichokifanya ndio uwezo wake umeishia hapo.

Hamuwezi Sabaya kwakuwa anatumwa na Magu ambaye ni boss wake.

Hata Jecha mnamlumu bure tu.

Yeye alisimamiwa na kina Mkapa, akaambiwa futa matokeo. Uwezo wa kukataa hana
 
Back
Top Bottom