Wakuu kuna hii kauli ya mkuu wa mkoa wa Kagera RC Kijuu kusema watumishi hewa wajiondoe, mi nashindwa kuelewa kwamba watumishi hewa ni watu walio hai au vipi?
Nakumbuka Rais Magufuli alipokuwa anazungumzia watumishi hewa alitolea mfano mtu ambaye alishakufa lakini analipwa mshahara, au mimi ndo nimemwelewa vibaya??
Chanzo: Mpekuzi
Nakumbuka Rais Magufuli alipokuwa anazungumzia watumishi hewa alitolea mfano mtu ambaye alishakufa lakini analipwa mshahara, au mimi ndo nimemwelewa vibaya??
Mkuu mpya wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu amewaagiza watumishi wasio na sifa za kuajiriwa kujiondoa kabla ya March 31 mwaka huu.
Kijuu alitoa kauli hiyo jana wakati wa Makabidhiano ya ofisi baina yake na mkuu wa mkoa wa zamani,John Mongella ambapo alisema kwamba Tanzania inawatumishi hewa zaidi ya 2000, hivyo ana imani hata Kagera wapo.
"Hao watumishi hewa endapo watang'ang'ania kubaki katika vitengo walivyopo nitawashughulikia wahusika wakuu wa vitengo hivyo," alisema.
Aidha, aliagiza wakuu wote wa wilaya za mkoa huo kusimamia uundwaji wa mabaraza ya usuluhishi kuanzia ngazi za kata hadi mkoa ili kusimamia haki za wananchi.
Pia aliwataka watumishi wa serikali mkoani humo kufahamu maudhui ya "Hapa Kazi Tu", kwa kufanya kazi kwa kasi,haraka, nguvu, maarifa na uadilifu.
Aliwataka kutosubiri kusukumwa, lakini wajitambue wao ni akina nani na wanapaswa kufanya nini kutokana na majukumu waliyopewa.
Alisema ili kufikia lengo la Rais John Magufuli la kuwatumikia wananchi kwa uaminifu ni lazima kushikiria uadilifu na kutambua kwamba watumishi wapo kwa ajili ya kutoa huduma kwa jamii.
Chanzo: Mpekuzi