Tetesi: RC Gambo adaiwa kupigwa kwenye Mkutano wa CCM Arusha

Status
Not open for further replies.
Kuna tetesi zinadai kwamba, Mkuu wa Mkoa WA Arusha Mrisho Gambo amepokea kipigo kutoka kwa Katibu wa Ccm Mkoani Arusha Elias Mpanda Mara baada ya kulazimisha wajumbe wasiohusika kuingia kikao cha kamati ya siasa mkoa ambao yeye mkuu wa mkoa ni mjumbe lakini huku akilazimisha waingie kamanda wa TAKUKURU ARUSHA na AFISA USALAMA TAIFA MKOA ambao kiitifaki si wajumbe wa kikao hicho.

Gambo amepokea kichapo hicho na kumsababisha kuvimba pua na Mdomo baadaya ya kulazimisha wajumbe hao ambao kimsingi si wajumbe kutaka washiriki kiako na kuanza kumporomoshea matusi ya nguoni katibu wa mkoa ccm bwana Elias Mpanda,

hata hivyo baada ya kipigo kikao hicho kilichokuwa ofisi ya mkoa Arusha kilivunjika,baada ya kuvunjika mkuu wa mkoa alituma Askari wakuu akiwemo RCO wa Arusha kumkamata Katibu huyo lakini busara za RCO aliyekaa kikao na pande zote mbili kutuliza hasira zao.

Hata hivyo haijulikani kikao hicho kitafanyila lini tena huku Mwenyekiti akitafakari namna itakavyo endelea.

Gambo ambaye alipachika wagombea wake kila eneo lakini walishindwa na kambi ya mkiti aliyeshinda mh Sanare amekuwa kwenye wakati ngumu katika vikao hivyo.

Hadi sasa imekua siri kwa wanachama wa Chama cha mapinduzi Ccm Mkoa wa Arusha kuwa kitendo hicho ni cha aibu sana,
Msimamo wa kamati ya siasa ni kuwa wateule na viongozi wakuchaguliwa kutekeleza ilani ya chama badala ya kuingilia maamuzi ama kuendesha chama kwa mgongo wa uteuzi wao

Gambo alifika katika kikao kikao hicho na Afisa usalama wa Mkoa Rso pamoja na kamanda wa Takukuru Mkoa Wa Arusha
Kawaida ukipigwa gumi la pua mchuzi humwagika, huyu je?
 
Rc huwezi kumfananisha na mtu kama lema,ni mwenyekiti kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa ana dola ana mlinzi,unaanzaje kumpiga?
Eti Rco Katumia busara,Rc akisema kamata weka ndani ni amri
Halafu ccm ni chama tawala,kina haki kumuita afisa yoyote wa serikali kwa ajili ya kutoa ufafanuzi kikaoni

Kumbuka huo ni ugomvi wa ndani we mbiga, sio ugomvi na manyumbu EBO!!! (Mwenyekiti wa mkoa anaweza kuongea na mwenyekiti wa Taifa ambaye ni Rais, na Gambo anaweza kuongea na Rais moja kwa moja ambaye ni Mwenyekiti wa Chama! UMEZIONA BUSARA ZA RCO HAPO AMA BADO!!!!!!
 
Inawezekana ikawa kweli kuwa aliambulia ngumi jiwe kwani jamaa ana matusi ya kuudhi tena wakati mwingine ya nguoni! Namkumbuka kipindi kile alichokuwa mkuu wa wilaya ya korogwe alimtukana sana yule dada aliyekuwa mwanasheria wa wilaya kuwa ana degree ya chupi! Hata ningekuwa mimi ndiye katibu ningemfuata hadi nyumbani kwake tumalizane tu kibingwa!
 
Ukuta wa Mererani haumhusu, ukuta unazinduliwa Manyara, yeye kipigiwa Arusha, allegedly. Awepo asiwepo kwenye ukuta haigeuzi ukweli kama kapigwa au hajapigwa.

Kiongozi ambae ukisemekana umepigwa watu wanashangilia lazima ujipime unakosea wapi.

Warioba alipigwa nchi ikalaani na kuhuzunika. Msafara wa Mkapa ulipopolewa mawe Masaki jamii ikashangilia. Tujihoji, wajipime.
Hata kama kapigwa,shida iko wapi?!!yeye ni yesu? au Muhammad?apite hivi
 
Kuna tetesi zinadai kwamba, Mkuu wa Mkoa WA Arusha Mrisho Gambo amepokea kipigo kutoka kwa Katibu wa Ccm Mkoani Arusha Elias Mpanda Mara baada ya kulazimisha wajumbe wasiohusika kuingia kikao cha kamati ya siasa mkoa ambao yeye mkuu wa mkoa ni mjumbe lakini huku akilazimisha waingie kamanda wa TAKUKURU ARUSHA na AFISA USALAMA TAIFA MKOA ambao kiitifaki si wajumbe wa kikao hicho.

Gambo amepokea kichapo hicho na kumsababisha kuvimba pua na Mdomo baadaya ya kulazimisha wajumbe hao ambao kimsingi si wajumbe kutaka washiriki kiako na kuanza kumporomoshea matusi ya nguoni katibu wa mkoa ccm bwana Elias Mpanda,

hata hivyo baada ya kipigo kikao hicho kilichokuwa ofisi ya mkoa Arusha kilivunjika,baada ya kuvunjika mkuu wa mkoa alituma Askari wakuu akiwemo RCO wa Arusha kumkamata Katibu huyo lakini busara za RCO aliyekaa kikao na pande zote mbili kutuliza hasira zao.

Hata hivyo haijulikani kikao hicho kitafanyila lini tena huku Mwenyekiti akitafakari namna itakavyo endelea.

Gambo ambaye alipachika wagombea wake kila eneo lakini walishindwa na kambi ya mkiti aliyeshinda mh Sanare amekuwa kwenye wakati ngumu katika vikao hivyo.

Hadi sasa imekua siri kwa wanachama wa Chama cha mapinduzi Ccm Mkoa wa Arusha kuwa kitendo hicho ni cha aibu sana,
Msimamo wa kamati ya siasa ni kuwa wateule na viongozi wakuchaguliwa kutekeleza ilani ya chama badala ya kuingilia maamuzi ama kuendesha chama kwa mgongo wa uteuzi wao

Gambo alifika katika kikao kikao hicho na Afisa usalama wa Mkoa Rso pamoja na kamanda wa Takukuru Mkoa Wa Arusha
Aibu hizi tutaziweka wapi jamani,Magu mbona hatukuelewi na wateule wako hawa?Hivi tuseme TISS wameshindwa kabisa kukupatia watu ambao watakipa chama na serikali taswira nzuri.Ni aibu sana kama ni kweli.
 
Hapana PM ni no.3 kwa ukubwa kisha linafuata Baraza la Mawaziri in terms of political rulling, lakini kwenye executive powers, hata ma PS kwenye wizara ndio wakuu, where executive powers lies, ndio kwenye nguvu.

P
PM ni namba 4 namba Moja Rais namba mbili makamu wa Rais namba tatu Rais wa Zanzibar namba nne Waziri Mkuu kwa itifaki ya Tanzania
 
Rais ni mkuu wa the executive, ni head of state na amiri jeshi mkuu, mawaziri ni political appointee tuu, hawana executive powers, wakuu wa mikoa ni executive positions, waziri hapigiwi saluti, RC anapigiwa saluti.

Ma RC ndio wakuu wa kamati za ulinzi na usalama
ana tuma report yake direct to No.1. Waziri ni mtu mdogo in terms of power kumlinganisha na RC.
Japo structurally Waziri ni mkubwa, lakini application RC kimkoa ni mkubwa kuliko Waziri, huyu kwa mkoa ni rais wa mkoa, waziri sio rais wa popote. Hapa tunazungunzia powers na sio responsibilities.

P
Unaongelea itifaki ya nchi gani paskali? Hoja salute hata Mbunge anapigiwa salute, Jaji anapigiwa salute, inspector anapigiwa salute. Kwahiyo kupigiwa salute siyo hoja.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom