BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 654
- 1,598
Wakati Kariakoo ikitajwa kuwa kitovu muhimu cha biashara katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, jambo linalofanya kuwa lango muhimu la uchumi wa Taifa, kwa muda sasa mitaa mingi ya soko hilo imekuwa ikikabiliwa na changamoto ya chemba zinazotiririsha maji taka katika maeneo ya biashara pamoja na kwenye njia za watembea kwa miguu.
Kwa takribani mwezi mizima sasa, baadhi ya mitaa muhimu ya Kariakoo imekuwa ikikumbwa na changamoto hiyo, hususan njia ya kuingia sokoni (eneo la maegesho ya daladala za Masaki), pamoja na Msimbazi kwenye Barabara Kuu (mkabala na Kituo cha Polisi).
Hali ni mbaya katika maeneo hayo. Kibaya zaidi, maeneo hayo yamezungukwa kwa karibu na shughuli nyingi za kibiashara, huku magari yanayopita yakitimua maji hayo machafu, hali ambayo inahatarisha afya za wananchi.
Juzi, nikiwa mwenyeji wa rafiki yangu kutoka Rwanda aliyefika kununua bidhaa, aliniuliza swali muhimu ambalo limenisukuma kuandika kero hii. Aliniuliza: Kwani hakuna viongozi wanaosimamia Kariakoo, hususan suala la usafi?
Binafsi, kwa haraka nilifikiria uwepo wa Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya, DAWASA, na hata nikafikiria hadi Wizara husika. Nikajiuliza, je, mamlaka hizi zote zimeshindwa kuona kwa uzito changamoto hii? Kwa nini maji taka yazagae mitaani kwa kiwango hiki? Tatizo ni nini hasa?
Rafiki yangu huyo aliniongeza ufahamu akisema kuwa Kariakoo, kwa namna inavyotajwa kwa uzito na kwa jina kubwa ililonalo katika ukanda wa Afrika Mashariki, huku ikipokea wafanyabiashara kutoka maeneo mbalimbali, suala la miundombinu ya usafi linapaswa kupewa kipaumbele cha juu. Alisisitiza kuwa eneo hilo linazalisha mapato makubwa.
Niliungana naye kwa asilimia mia moja, hasa nilipokumbuka taarifa za TRA kuhusu makusanyo ya kodi yanayopatikana katika Mkoa huo wa Kikodi, bila hata kujumuisha mapato yanayokusanywa na Jiji.
Kiukweli, tunataka kuona uwajibikaji katika kushughulikia changamoto hii. Au kama tunasubiri kwanza magonjwa ya mlipuko yatokee ndipo tuchukue hatua, basi hilo liwekwe wazi ili wananchi tufahamu.