RC Chalamila naomba uiangalie Temeke

RC Chalamila naomba uiangalie Temeke

ZINDAGI

JF-Expert Member
Joined
Dec 5, 2015
Posts
1,118
Reaction score
1,437
Kwanza nikupongeze kwa kuteuliwa kuwa kiongozi mkuu wa mkoa huu wenye sura ya nchi, wewe ni kiongozi sahihi kwa mkoa huu wa DAr es Salaam.

Pili, katika kiindi kifupi ulichokaa tumeona umeenda kugusa maeneo yenye matatizo ya mkoa na humungunyi maneno, wanasema una hit the target.

Ombi langu kwako, tumeona umetembelea Wilaya za Ilala, kinondoni, sasa tunaomba uhamie Temeke, hii wilaya haina hadhi ya kuwa katika hili jiji, matatizo ni mengi huku;
1. Usafi ni tatizo kubwa sana, hakuna vitendea kazi, taka zinakaa mpaka mwezi hazijazolewa.
2. Miundo mbinu ya barabara za mtaani ni horrible, barabara zimekua ndio magereji.
3. Uchafu wa mazingira ni mkubwa mno, matairi ya magari yanachomwa hapo Temeke mwisho, afya zetu zinaathirika kwa moshi mzito unaotanda usiku.
4. Baraara zinazotengemezwa Temeke ni za kiwango duni ukilingamisha na zile za Kinondoni hakuna usimamizi.
5. Mitaa imekua ndio sehemu ya kuegesha malori, watoto wetu hawana hata sehemu za kucheza.

Tukuombe uje uweke kambi huku ujionee mwenyewe hali halisi.
 
Yule Jokate alikuwa wilaya gani hapo DAR?
Hizo changamoto ni kubwa kuliko Chalamila mwenyewe.
 
Mvunja nchi mwananchi!fanyeni usafi acheni ,acheni kuchoma matairi! mwenzenu Chalamila atakuja hapo nusu saa ataongea ongea huyooooo anarudi kwake kula upepo wa bahari
 
Mvunja nchi mwananchi!fanyeni usafi acheni ,acheni kuchoma matairi! mwenzenu Chalamila atakuja hapo nusu saa ataongea ongea huyooooo anarudi kwake kula upepo wa bahari
Usafi tunafanya, taka tunakusanya, lkn wazoaji wakuzipeleka dampo hakuna, hatuoni magari ya taka hata kama tunalipa kila mwezi
 
Back
Top Bottom