Wanaendesha nchi kihuni sana. Jana nilisema humu ndani, wanataka faida za curfew bila kutangaza hiyo curfew waziwazi.
Wanasema wanatoa ushauri ila ni amri ili baadae warudi kama hivi wajisifu nchi ilikuwa imetulia na hatukuwalazimisha watu wakae ndani.
Kesho utawaambia watu tena kwamba unawashauri wakae ndani watakugomea maana watakumbuka uliwahi kusema hivyo baadae ukawaambia haukuwalazimisha kukaa ndani.
Nchi ina ombwe kubwa la kiuongozi. Shida ni kwamba, mtaongoza nchi kwa njia za janja janja kama hivi mpaka lini?