PAYE
JF-Expert Member
- Jun 19, 2025
- 354
- 395
Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama ya Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu, ametoa wito kwa wananchi wa mkoa huo waliojiandikisha kujitokeza kwa wingi kupiga kura Oktoba 29, 2025, bila kuwa na hofu yoyote.
Babu ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, ameyasema hayo mjini Moshi, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari akiwa na Kamati ya Usalama ya Mkoa, ambapo ameelezea suala la usalama katika kipindi cha uchaguzi mkuu na kuongeza kuwa mkoa huo umejipanga kuhakikisha wananchi wanatimiza wajibu na haki yao ya kikatiba kwa kupiga kura.
Amewahakikishia wananchi wa Kilimanjaro usalama kwa asilimia 100, hivyo amewasihi wajitokeze mapema kwenye vituo walivyojiandikisha na baada ya kukamilisha zoezi hilo warudi nyumbani kuendelea na shughuli zao za maendeleo.
Kwa upande wake, Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Kilimanjaro, Gasper Ijiko, ameeleza kuwa vituo vya kupigia kura vitafunguliwa mapema saa 12 asubuhi na maandalizi yanaendelea vizuri, hivyo wananchi wote wenye sifa wajitokeza kwa wingi kupiga kura siku ikifika.