RC Arusha amsweka ndani mkandarasi

buswelu moja

JF-Expert Member
Aug 24, 2014
226
147
Mkuu wa mkoa wa Arusha, mrisho Gambo ameamuru mkurugenzi wa kampuni ya ukandarasi ya TANCHI BROTHERS, Zhong Hong awekwe mahabusu kwa muda wa saa 24 kutokana na kusuasua kukamilisha mradi wa ujenzi wa ofisi za mamlaka ya maji mkoani Arusha.

Mbali na mkurugenzi huyo pia aliamuru wasaidizi wake wawili ambao ni watanzania wawekwe ndani.

Agizo hilo limefuatia baada ya Rc Gambo juzi kufanya ziara ya kutembelea mradi huo ambao unatarajia Kukamilika February 2020 na kukuta mradi huo ukisuasua jambo lililomlazimu kumwita ofisini mkandarasi huyo jana na kisha kuamuru awekwe mahabusu.
Screenshot_20191112-115952.jpeg
 
Hela amelipwa huyo mkandarasi? Akishawekwa ndani hizo ofisi zitakamilika?
 
Ndio lugha inayoeleweka kwa hawa wakandarasi, hivi sasa wengi wanajituma kupita maelezo maana hawavumiliwi tena, hii yote kwa ajili ya utawala mpya ambao unazingatia matokeo kushinda ngonjera.
Kule Tabora Mwaniri hawapi nafasi, wakikimbilia Dar wanakutana na Makonda, kazi zinakwenda, awamu hii ukipokea kandarasi lazima ujiandae kukamilisha kwa wakati ufaao na pia uhakikishe ubora.
Afrika itaamka, waje wapate darasa Tanzania namna gani ya kubadilisha nchi kwa kipindi cha muda mfupi.
 
Back
Top Bottom