Raza amuunga mkono Mengi kukemea ufisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Raza amuunga mkono Mengi kukemea ufisadi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ochu, Sep 8, 2008.

 1. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #1
  Sep 8, 2008
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Na Joseph Mwendapole

  Mfanyabiashara maarufu wa Zanzibar, Mohamed Ibrahim Raza, ameunga mkono kauli iliyotolewa na Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi, ya kukemea kundi la mafisadi linalotaka kudhoofisha watu wanaomuunga mkono Rais Jakaya Kikwete katika vita dhidi ya ufisadi.

  Akizungumza na Nipashe jana, Raza alisema endapo Watanzania wataamua kukaa kimya kuhusu suala hilo ni dhahiri madhara yake yatakuwa makubwa.

  Alisema yeye binafsi anaunga mkono jitihada zinazochukuliwa na Rais Kikwete katika kushughulikia masuala ya rushwa na ufisadi hivyo aliwataka Watanzania wengine wamuunge mkono.

  `` Tusikae kimya hata kidogo, suala la wizi na ufisadi ni janga kubwa, lazima Watanzania tuache woga na tuwe na wajibu wa kuwasema watu wanaotaka kuliangamiza Taifa kwa wizi wa fedha za umma,`` alisema Raza.

  Aliongeza kuwa huduma nyingi muhimu kama shule, barabara na hospitali haziwafikii wananchi walio wengi hivyo kuna umuhimu wa kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma.

  Alisema udanganyifu wa wazi wazi ulifanyika katika mkataba wa kampuni ya kufua umeme ya Richmond na kuisababishia serikali hasara kubwa.
  Alisema fedha hizo zingeweza kutumika kuwaletea maendeleo wananchi ambao wengi hawapati hata huduma ya maji safi.

  ``Kama Mengi anathubutu kusema na sisi Watanzania wengine tusisite kumuunga mkono na tusipofanya hivyo madhara yanakuja kwetu sote kwani huduma muhimu hazitapatikana,`` alisisitiza Raza.

  Kadhalika, Raza aliongeza kuwa hivi sasa makampuni mengi yameanza kuingiza chakula kibovu kisichofaa kwa matumizi ya binadamu na kuwauzia wananchi.

  Alisema jitihada za pamoja zinahitajika kuhakikisha wafanyabiashara hao wasio na uzalendo wanafichuliwa kwa maslahi ya umma.

  Raza alisema serikali inapaswa kuwafikisha mahakamani watu walioiba fedha kwenye Akaunti ya Malipo ya Nje (EPA) hata watakaporejesha fedha walizoiba.

  Hivi karibuni, Mengi alisema limejitokeza kundi la mafisadi na la waongo na vibaraka uchwara lenye nia ya kuhakikisha kwamba ushupavu na uadilifuwa wale wanaomuunga mkono Rais Kikwete katika vita dhidi ya ufisadi unadhoofishwa.

  * SOURCE: Nipashe
   
 2. F

  Fisadi Mtoto JF-Expert Member

  #2
  Sep 15, 2008
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 639
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Raza nae ni mtu wa kusema mtu kweli wakati yeye nae hana maadili yeyote yale.alizoea kuingiza vipikipiki bila kulipia ushuru sasa wamempiga chini analia nini tena.
   
Loading...