Ray C afunguka kuhusu utumwa wa Dawa za kulevya

Ray C afunguka kuhusu utumwa wa Dawa za kulevya

Mapengo 17

R I P
Joined
Mar 28, 2014
Posts
1,228
Reaction score
618
GWIJI wa muziki wa Bongo Flava, Rehema Chalamila, al-maarufu Ray C amekanusha vikali uvumi ambao umekuwa ukisambaa Tanzania na Afrika Mashariki kwa jumla kwamba amewahi kuwa na urafiki wa kimapenzi na Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania.

Hata hivyo, Ray C, alikiri jinsi alivyookolewa na Rais Kikwete kutoka katika janga la mihadarati baada ya rais huyo kupata habari zake katika vyombo vya habari. Msanii huyo ameanzisha kituo cha kuwafanyia marekebisho waathiriwa wa mihadarati ambao wengi wao ni vijana.

Swali: Uliingiaje katika matumizi ya mihadarati?

JIBU: Mpenzi wangu wa zamani aliniingiza katika janga hili. Sikujua mapema kwamba alikuwa mraibu wa mihadarati nilipokutana naye kwanza. Wala sikujua tofauti ya bangi na mihadarati mingine kutokana na ugeni wangu. Polepole nilijikuta nikitumia dawa za kila aina. Mwili wangu ulianza kudhoofika huku nikishindwa kukaa bila kutumia mihadarati. Mwili wote ungeniuma kama ningekosa kutumia.

Swali: Unakumbuka ulitumia kiasi gani cha pesa kwa wiki katika hiyo mihadarati?

JIBU: Kilikuwa kiasi kikubwa mno ambacho siwezi kukikumbuka. Machozi hunilengalenga kila ninapojaribu kukumbuka. Wakati mmoja ilinibidi kuuza nyumba yangu, nikafunga maduka na kuuza mali yangu nyingi ili nipate pesa za mihadarati. Nilijifunza kwamba haijalishi kwamba u tajiri kiasi gani. Ukijiingiza katika matumizi ya mihadarati lazima hatimaye ufilisike.

Swali:Je, familia yako ilijua kuwa ulikuwa umetumbukia katika janga la matumizi ya mihadarati?

JIBU: Nilijaribu sana kujificha nikitaraji kuwa hali yangu haingetambulika. Hata hivyo, mamangu alitambua mabadiliko niliyokuwa nayo. Sura yangu haikung’ara tena, nikapoteza hamu ya kula na zaidi ya hayo nilikuwa mwepesi sana wa kukasirika. Mama aliniita na kunishauri kuukata urafiki na mpenzi wangu ambaye alimjua kama mzoefu wa kutumia mihadarati lakini nikapuuza ushauri huo.

Swali: Uliamua lini kuacha matumizi ya mihadarati?

JIBU: Ulikuwa mwaka 2012 ambapo niliamua ama nijiue au niende jela. Nilikuwa nimechoshwa na utumwa wa mihadarati. Sikuona maana ya maisha ikiwa kila senti niliyoipata iliingia katika mihadarati. Niliachana na mpenzi wangu. Kama mamangu hangekuwepo kunishughulikia sasa hivi stori ingekuwa tofauti.

Swali: Je, uliweza kuacha matumizi hayo ya mihadarati tu ghafla kama umepunguza tu kama watu wasemavyo?

JIBU: Wajua watu wanayo mengi sana ya kusema na huwezi kuwazuia. Rais Kikwete alipojitolea na kunisaidia nilijikaza kisabuni na kuachana na mihadarati. Nilitaka kuachana na aibu yangu ya kutajwatajwa hadharani kama mwathirika wa matumizi ya mihadarati na Mola ameniwezesha kufikia lengo langu.

Swali: Je, Rais Kikwete alijuaje shida yako na kunao ukweli wowote kwa mlikuwa na urafiki wa kimapenzi?

JIBU: Sina hakika sana ila nakisia tu kwamba ilikuwa kupitia katika vyombo vya habari hasa magazeti na radio baada ya mamangu kuzungumza na waandishi wa habari. Kuhusu urafiki hilo nakanusha kabisa kwa maana ilikuwa mara yangu ya kwanza kumwona akiwa karibu nami na ninamshukuru sana kwa ukarimu wake ambao umeniweka hai hadi leo. Nitamwombea Mungu ambariki katika kila alifanyalo.

Swali: Je, kumekuwa na mabadiliko yoyote kwako tangu uache mihadarati?

JIBU: Sasa ninaishi maisha ya uhakika. Najisikia kuwa mwenye afya. Lakini sina imani tena na wanaume na nitakaa kwa muda bila kuwa na urafiki nao na ikiwa ni lazima urafiki huo uwepo basi nitamtafuta mwanamume wa miaka 60 na zaidi. Sitataka urafiki na vijana tena kwani huo ndio ulioniingiza katika mateso niliyopitia.

Swali: Umekaa miaka kadhaa bila kuwa katika ulingo wa muziki. Huoni kuwa umesahaulika?

JIBU: Umahiri wangu nauona uko pale pale. Ni kweli kuna mabadiliko makubwa na mazuri katika muziki chapa Bongo Flava. Hata hivyo, kwa vigogo kama sisi tunasalia pale pale; tunaona wageni wakija na kupita kama moshi tu huku sisi tukisalia pale pale tukiendelea kuimarika tu. Tayari nimetayarisha albamu mpya na nasubiri wakati mwafaka kuizindua.

Swali: Umefungua kituo cha Ray C Foundation kusaidia walioathiriwa na mihadarati. Je, unatarajia kumsaidia mpenzi wako wa zamani pia?

JIBU: Ni hiari yake. Siwezi kumlazimisha. Ni vigumu sana kumlazimisha mtu kubadilisha mwenendo wake. Hata hivyo, akija nitakuwa tayari kumpokea na kumsaidia.

Swali: Je, ni kweli wanavyodai mashabiki wako kuwa umeichubua ngozi yako ili uonekane mweupe zaidi?

JIBU: Hata kidogo na wala sidhamirii kufanya hivyo karibuni. Kunawiri kwa ngozi yangu kwatokana na afya nzuri ambayo imeanza kurudi hivi karibuni.

Swali: Tumekaa sana bila kitu kipya kutoka kwako. Unatupa nini hivi karibuni?

Jibu: Tayari nimerekodi albamu mpya ingawa meneja wangu anasisitiza tusubiri hadi wakati mwafaka uwadie ndipo tuachilie ngoma hizo. Nina hakika mtazifurahia.

Chanzo: Eddy Blog
 
Hatua nzuri kabisa maishani na Mungu akusaidie ili uweze kusaidia na wengine kujinasua na utumwa wa dawa za kulevya na maovu mengine
 
Huyu akae apike ubwabwa tu kwenye mgahawa wake mwananyamala hana cha kushauri mtu hapa
 
Huyu akae apike ubwabwa tu kwenye mgahawa wake mwananyamala hana cha kushauri mtu hapa
Kumbe ile single yake ya.mama ntilie, kumbe ndiyo fani yake mpya rasmi, baada ya kulostishwa na uteja wa kubwia unga?
 
Well done...kudos kwa kufanikiwa kuacha ray C..

But huyu profesa kikwete me simuelewi guyz...lets reason pamoja maybe wanajamvi mnaweza kunisaidia au kuniweka sawa

Kikwete az a sovereign state president anapongezwa vipi kwa kufanya rehab ya mtu mmoja tena maarufu?ray c ana haki ya kushukuru personally but taifa linaachwa vipi ob this matter?inawezekana kuna watu wengine amewasaidia on this but yeye kama rais...literally a most powerful person in the country anatakiwa kuzuia uingizaji wa haya madawa na kusaidia vijana na kizazi chote cha tanzania...na kwa bahati nzuri alisha state kuwa abnawajua drug dealers wote kwenye media...na aka hint kuwa hadi viongozi wa dini wapo,,,anakujaje kuanza kuanza kudeal na waathirika instead of controlling the importation of these drugz(afterall most of njia wanazotumia kuingiza zinajulikana wazi)

Hii ni aibu...je ni watanzania wangapi nguvukazi wanaoteketea coz of these drugz?je ni vijana wangapi ambao hawawezi kufikiwa na rehabiliation programmes?hii ni aibu kwa serikali..kikwete should deal with the source and sio kutafuta publicity through dealing with outcomes tena na very low %

Kazi ya rehab awaachie ngo's na taasisi za kidini
 
Hii ni aibu...je ni watanzania wangapi nguvukazi wanaoteketea coz of these drugz?je ni vijana wangapi ambao hawawezi kufikiwa na rehabil
 
Well done...kudos kwa kufanikiwa kuacha ray C..

But huyu profesa kikwete me simuelewi guyz...lets reason pamoja maybe wanajamvi mnaweza kunisaidia au kuniweka sawa

Kikwete az a sovereign state president anapongezwa vipi kwa kufanya rehab ya mtu mmoja tena maarufu?ray c ana haki ya kushukuru personally but taifa linaachwa vipi ob this matter?inawezekana kuna watu wengine amewasaidia on this but yeye kama rais...literally a most powerful person in the country anatakiwa kuzuia uingizaji wa haya madawa na kusaidia vijana na kizazi chote cha tanzania...na kwa bahati nzuri alisha state kuwa abnawajua drug dealers wote kwenye media...na aka hint kuwa hadi viongozi wa dini wapo,,,anakujaje kuanza kuanza kudeal na waathirika instead of controlling the importation of these drugz(afterall most of njia wanazotumia kuingiza zinajulikana wazi)

Hii ni aibu...je ni watanzania wangapi nguvukazi wanaoteketea coz of these drugz?je ni vijana wangapi ambao hawawezi kufikiwa na rehabiliation programmes?hii ni aibu kwa serikali..kikwete should deal with the source and sio kutafuta publicity through dealing with outcomes tena na very low %

Kazi ya rehab awaachie ngo's na taasisi za kidini

Kimafia mafia, ukishafanya biashara chafu sana unatakiwa kutoa sadaka kidogo na kusaidia masikini ili kusafisha jina.

Ndicho alichokuwa anafanya Kikwete hapo.

Kashaachia madawa yaingie kwa sana bongo, alikuwa anatafuta optics tu za kuonyesha Kikwete anajali.

Danganya toto.
 
Kimafia mafia, ukiahafanya biashara chafu sana unatakiwa kutoa sadaka kidogo na kusaidia masikini ili kisafisha jina.

Ndicho alichokuwa anafanya Kikwete hapo.

Kashaachia madawa yaingie kwa tano bongo, alikuwa anatafuta optics tu za kuonyesha Kikwete anajali.

Danganya toto.

Hii nchi ni shida mkuu
 
Hy tiba ya METHADONE inayotolewa na Taasisi yake ni hatari kwa afya ya watumiaji wa dawa za kulevya kwa sababu kitaalum binadamu hatakiwa kutegemea kumeza vidonge (pills) manake aina yyt ya dawa ikitumiwa kwa muda mrefu inakuwa ADDICTIVE KWA MTUMIAJI ili kukidhi haja yake ya kuishi so baada ya muda hawa jamaa watakuwa dependency kwa hizo dawa kama walivyokuwa wakitegemea dawa za kulevya mf: heroine, cocaine, bangi, khats, etc . Namshauri methadone itumike kwa kipindi fulani then mwathirika aanze kitu kiitwacho NARCOTICS ANONYMOUS OR N.A katika eneo lake ambazo ni fellowship za walikuwa waathirika na hivi sasa wanaishi bila matumizi ya dawa hizo, hawa ukutana katika maeneo mbalimbali na kujengana uwezo wa kuweza kuishi bila matumizi ya methadone+illicit drugs. Kwa maelezo zaidi tuwasiliane kwa email: rnelsontz@yahoo.com
 
Open the eyes of my heart, Lord
Open the eyes of my heart
I want to see You
I want to see You
Open the eyes of my heart, Lord
Open the eyes of my heart
I want to see You
I want to see You
To see You high and lifted up
Shinin' in the light of Your glory
Pour out Your power and love
As we sing holy, holy, holy
Open the eyes of my heart, Lord
Open the eyes of my heart
I want to see You
I want to see You
Open the eyes of my heart, Lord
Open the eyes of my heart
I want to see You
I want to see You
To see You high and lifted up
Shinin' in the light of Your glory
Pour out Your power and love
As we sing holy, holy, holy
To see You high and lifted up
Shinin' in the light of Your glory
Pour out Your power and love
As we sing holy, holy, holy
To see You high and lifted up
Shinin' in the light of Your glory
Pour out Your power and love
As we sing holy, holy, holy
Holy, holy, holy
We cry holy, holy, holy
You are holy, holy, holy
I want to see you
Holy, holy, holy
Holy, holy, holy
You are holy, holy, holy
I want to see you
Holy, holy, holy
Holy, holy, holy
Holy, holy, holy,
I want to see you
Holy, holy, holy
Holy, holy, holy
Holy, holy, holy,
I want to see you
Holy, holy, holy
Holy, holy, holy
Holy, holy, holy,
I want to see you
Holy, holy, holy
Holy, holy, holy
Holy, holy, holy,
I want to see you
Holy, holy, holy
Holy, holy, holy
Holy, holy, holy,
I want to see you
Holy, holy, holy
Holy, holy, holy
Holy, holy, holy,
I want to see you
 
Back
Top Bottom