Nimepigiwa simu jioni hii na jamaa yangu akiwa mgodini, amebahatika kupata kipande cha dhahabu. Shida yake kubwa ni kujua soko la dhahabu hapa Dar likoje? bei kwa gram moja ni shilingi ngapi?
Unawezaje kupata kipande cha dhahabu kama tanzanite?,dhahabu si inapatikama kama particles ndogondogo sana kwenye mchanga?,hilo pande la raw gold huyo jamaa katoa wapi sasa?.,au changa la macho?
Mkuu kwa jinsi navyo ijua Dhabu haipatikani kama kajiwe au tanzanite ,gold hadi ije tokea gold ina pitia process kadha ndio mwisho ije kuwa gold,mchanga unachukuliwa unao onekana unagold then una chekechwa kwa kutumia dawa kwa wenye machimbo makubwa wadogo wadogo hutumia chumvi,ina ozeshwa yani ina viprocess sana mwisho wa siku mecury inatumika pia nadhani ku tenganisha sikumbuki vizuri kwenye hii process ndio na silver inatoka hapo hapo. ndio maana Gold nyingi ina kuwa katika bars kama vitofali vidogo.na hiyo inatokana badaa ya zile chenga chenga zilizo patikana kutoka kwenye process ku yeyushwa ,ila gold huwezi chimba na kupata ki jiwe kama tanzanite ,tanzanite ndio unaweza sema umepata kajiwe kako ka ajabu ajabu ,ila gold lazima upitie process ndio ije kuwa goldKwanini isipatikane inapatikana kama kawaida kwani unayeyusha Kisha unapata kipande kizama