KIDOLEGUMBA
JF-Expert Member
- Apr 17, 2013
- 498
- 110
hebu nisaidie kuisoma hii picha.. ina maana siku za katikati ya wili/ mwezi mtu anaweza kuwa na hot date so ana-reserve kwa huyo date wake?
ni makubaliano tu baina yenu wawili....
Habar wadau, Kwa waliondani ya ndoa na wengine wanaoishi pamoja wapenzi wa siku hizi wamekuwa na tabia ya kuweka ratiba ya tendo la faragha /ndoa mfano wengine kwa wiki mara moja, kwa mwezi mara 2 .
Je ni sahihi kwa wapenzi/wanandoa kuwa na ratiba ya tendo la faragha/ndoa au si haki kuwekeana ratiba?
he!!hata maofisini kuna vikao vya dharura...flexible schedule....wa kuwepo kwa ratiba? kwa iyo ukizidiwa kabla ya siku husika inakuaje hapo?
Tendo la ndoa halina ratiba jombaa, ufanyaji wake unategemea hasa jinsi mnavyoishi!! Kama mnapendana, mnaelewana na mnapokuwa nyumbani mnaishi kimapenzi kweli (romantic) kama kuoga pamoja, kupika pamoja na vitu kama hivyo mtajikuta automatically mnalifanya mara kwa mara sababu ya ule ukaribu na kila mtu akafurahia sana!!
Ila kama mkirudi home kila mmoja na time yake mtajikuta mnakwenda kama kwa ratiba vile, siku tano hamjagusana na mkigusana leo mnakaa tena wiki so inakuwa kama karatiba fulani hivi.
Badilika ufaidi ndoa yako, amri zako kazini kwako nyumbani unakuwa mpolee na mkarimu kwa mwenza wako!!
Mmmh! Ratiba ? Ngoja nikikua!!
Hapo ni kweli mkuu ila siku hizi Wanandoa wanakuwa bize kusaka njuruku kiasi kwamba romance inanafasi ndogo sana kwa siku za wiki haswa jumatatu hadi jumamosi! Uchovu na Stress za Ugumu wa maisha pia huondoa kabisaaa romance ndani ya nyumba, Maji yenyewe yanatoka kwa wiki Mara moja mtaani huku.
Tendo la ndoa halina ratiba jombaa, !
Siyo reason kiviilee!! Mkeo/mumeo ndiyo faraja yako, pambana mchana kutwa lakini unapofika kwa mwenzi wako stress zote tupa kule mnaingia katika mambo mengine na familia yako!! Ndo mana mnakufa siku si zenu kwa kuendekeza stress 24/7!! Wakati unaweza kumaliza stress kwa kumsaidia mkeo kukaanga kaanga huku mkitaniana na kucheka pamoja!!
Usipooga ndo unamwogopa mkeo?? Asipojua unanuka kikwapa unataka adhani unanuka vitunguu??