Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,253
- 36,508
Wiki chache zilizopita nilifanikiwa kumuona na kumsikiliza Maalim Seif katika kipindi cha luninga cha ahsubuhi akielezea yanayojiri Zanzibar na Chama chake cha CUF. Kituo hiko hiko kesho yake walimualika Prof Lipumba na kuhojiana naye kuhusu yale waliyomuuliza Seif.
Hayo yamejiri kama matokeo baada ya washirika wa Seif katika UKAWA kuamua kuingilia uhuru na demokrasia ndani ya chama cha CUF huku ilihali wanapalilia mgogoro na kuutukuza ubaguzi mkubwa na wa wazi anaoufanya Seif na wenzake.
Naam, UKAWA kirefu chake ni Umoja wa Katiba ya Wananchi ambapo lengo lake lilikuwa ni kuhakikisha maoni ya wananchi katika Katiba mpya (rasimu ya Warioba) yanaheshimiwa. Lakini kilichotokea ni hadaa kwani hata kabla hawajaunda huo Ukawa tayari viongozi hao walisimama kidete kuipinga rasimu ile ile kabla haijawasilishwa Bunge la Katiba.
Baada ya UKAWA kuundwa ikaonekana ndiyo namna pekee ya kuunganisha nguvu ya kisiasa dhidi ya CCM ili kuitoa madarakani. Lakini ukiwauliza watukufu wa Ukawa nini malengo yao watakujibu kwa kuhubiri mapungufu ya CCM na kasoro zake huku wakiapiza kurekebissha changamoto hizo. Kwa sisi wenye akili tunag'amua kwamba hapo hakuna jipya kwani unaposema unatarajia kutatua matatizo bila kuwa na mpangokazi ni sawa na kutegemea kudra kwenye jambo ambalo ni lazima juhudi ifanyike.
Tunashuhudia leo namna injini za propaganda zinavyofanyakazi mitandaoni na vyombo vya habari katika kuchafuana wenyewe kwa wenyewe na wanavyojiundia udiktekta kwenye vyama vyao. Unapokuwa katika vyamba vya UKAWA na ukafanikiwa kuwa kiongozi wa umma basi wewe unakuwa na cheo cha kuwa msemaji wa chama na UKAWA. Hakuna nidhamu wala mpangilio.
Unakuta kiongozi anaongea maneno ya hovyo hata kufikia kiwango cha kutukana lakini hakuna anayekemea wala kuwarejesha katika mstari.
Badala ya kuunga mkono maendeleo, leo hii UKAWA imekuwa mstari wa mbele kupinga maendeleo na hata kupropagate dhidi ya mipango yote ya serikali kuwaletea maendeleo wananchi.
Ikumbukwe, Dr. Slaa alijitoa kwa kiwango cha juu kujenga upinzani wenye tija lakini alipoona kuna gia mbovu zilizolazimishiwa kubadilishiwa hewani akajiweka pembeni na hawakumuacha hivi hivi walimtukana na kumdhalilisha vya kutosha.
Leo wanapambana na Lipumba ambaye ni muasisi wa huo umoja wao
Wasichokijua wananchi ni kuwa injini nyuma ya mchezo huu wote ni Lowassa na Mbowe ambao kila mmoja kwa wakati wake alitumia njia za kuchafua wenzake wanaoonekana wana juhudi za kuimarisha vyama walivyokuwemo.
Mimi ninachokijua ni kwamba UKAWA imebaki jina, imekuwa ni kigenge cha kupata public sympathy na siyo tanuru la kupika viongozi na kuleta utunduizi wa hoja za kuwasaidia wananchi.
Wanadandia matukio
wanadandia hoja
wanadandia sera
wanadandia treni kwa mbele