LUS0MYA
JF-Expert Member
- Aug 4, 2011
- 866
- 1,110
Nimesikiliza kwa makini maelezo ya mheshimiwa judge Warioba kuhusu muundo wa muungano.Nakubaliana na maelezo kuwa waasisi walituachia nchi moja na serikali mbili.Lakini hali ya sasa kuna nchi mbili na serikali mbili.Sikubaliani na conclusion kuwa muundo wa serikali tatu ndio suluhisho!dhamira ya wazi kwa Zanzibar katika muungano haipo na wametumia baraza la wawakilishi kubadilisha mambo wanayotaka hata kwa kuvunja katiba!itakapopatikana bunge la Tanganyika mambo yanayofanywa na baraza la wawakilishi yatajirudia kwani hata Tanganyika zipo kero nyingi sana lakini hakuna pa kusemea.Kifupi Dhamira ya Muungano inaonekana kutokuwepo!Nionavyo mimi Katika serikali tatu muungano utavunjika na hata huu wa serikali mbili utadunda tu angalau kama CCM ipo madarakani.Kura ya maoni zanzibar na Tanganyika ni kitu cha muhimu kuona dhamira za wananchi wa nchi hizi kuhusu muungano!