Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 3,620
- 6,510
Tanzania imekuwa na ujinga mmoja ambapo rasilimali za nchi zimekuwa zinatumika kumlinda, kumtetea na hata kufungulia mashtaka watu kwa kesi binafsi za kiongozi.
Unaweza kukuta mtu anachapisha jambo fulani kuhusu kiongozi fulani, ambalo labda jamii, muhusika au vyombo vya serikali vinalitafsiri ni kashfa, kumvunjia heshma, nk.
Badala ya yeye kiongozi mwenyewe kufungua kesi binafsi, atatumia Polisi, DPP na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kumkamata na kumfungulia mashtaka mtu yule kwa makosa mengine (utasikia makosa ya kimtandao, uchochezi, uhujumu uchumi, nk.) wakati hapo ilitakiwa kiongozi atafute Wakili binafsi na kufungua kesi ya madai.
Huu ulikuwa ni utangulizi. Twende katika hoja ya uzi huu.
Nia ya uzi huu ni kukumbusha kuwa iwapo kuna mtu au watu watafunguliwa mashtaka yoyote katika Mahakama ya ICC kuhusiana na matukio ya MO29, kesi hizo zitawahusu wao binafsi na uhusika wao katika matukio yale.
Rasilimali za nchi hazitakiwi kutumika kuwatetea wala kuwalinda watu hao katika kesi hizo. Kama wataamua kumtumia Wakili Kibatala litakuwa jambo jema ili pesa ibaki hapa hapa nchini.
Haitakiwi pesa na rasilimali zingine za nchi kutumika kulipia wanasheria wa ndani au nje ya nchi kwa ajili ya utetezi wa watu hawa.
Ujumbe huu umfikie CAG!