Rasilimali asili za nchi ni nyara ya serikali? Mnatufundisha tuziimbe ila sio thamani yake ili mzifaidi nyie tu?

sifi leo

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
5,013
8,369
Asubuhi ya Leo nimeamka na kumkumbuka mwalimu wangu Mwakitwange aliyetokea chuo cha ualimu Katoke akiwa amevaa gwanda za JKT Enzi hizo.

Simkumbuki alinifundisha somo gani ila nakumbuka tu alikuwa akinikimbiza mchaka mchaka kila Jumatatu asubuhi huku alinifundisha tuimbe kawimbo Ka......

Mbuga za wanyama Tanzaniaaaaaaa ya Kwanza ni Serengeti, Ngorongoro, Mikumi ............. Sijui na ninnnnni? Za watanzania oyeeeeeee!

Nimejiwa na swali je Sisi tulifundishwa kuimba hizi rasilimali zetu tu ili tujue zipo Ila thamani yake inatakiwa kujulikana kwa watawala wetu?

Ni mitaala hiyo inayowapa kiburi viongozi wetu kujiona yakuwa Mali hizi ni zao ndio maana wanasaini mikataba ya ovyo dhidi ya rasilimali zetu.
 
Back
Top Bottom