Maendeleo miaka 50 ya Uhuru sio gift wala suprise kwa waTanzania. Ni wajibu, tuache sifa za kijinga

Ta Muganyizi

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
5,360
2,720
Kuna baadhi ya Watanzania wenzangu wananishangaza na kunisikitisha sana. Na hii ni pale wanapo hadaliwa na viongozi wa chama na serikali iliyoko madarakani kuhusu mafanikio yaliyopatikana tangu mwaka 1961 tulipopata Uhuru hadi leo. Utakuta watu wanatoa takwimu za ajabu kwa kuwataja wataalamu wa kada mbalimbali kuwa walikuwa idadi hii - sasa hivi ni idadi hii, mara shule zilikuwa idadi hii- sasa hivi ni idadi hii, mara barabara za lami zilikuwa kadhaa za kilometa kadhaaa- na sasa hivi ni kilometa kadhaaa.

Utakuta Watanzania wenzangu wanatikisa vichwa kwa kukubali kwamba kweli tumesonga mbele. Mwanasiasa mwingine anajivunia maendeleo kwa kueleza idadi ya simu za mchina zilizoko vijijini ambazo zinapiga mziki mzuri na mawasiliano vilevile.

Labda wengine mtanishangaa kwa kudhani kuwa mimi nakataa kwamba hatujasonga mbele. Pamoja na kusonga mbele kunakoonekana mimi sishangai hata kidogo wala sioni Suprise ya kufanya sherehe kubwa eti miaka 50 ya Uhuru. Kwa yeyote anayedanganywa na takwimu za vitu vilivyoongezeka inabidi ajue kwamba ( kwa mujibu wa vitabu vingi zaidi ya 50 nilivyosoma vya sayansi ya jamii) ni kuwa "Any society is dynamic" .Yaani ni kwamba kila jamii ya mwanadamu lazima ishuhudie mabadiliko kadri siku zinavyozidi kwenda mbele. Utake usitake lazima mabadiliko yatokeee. Kwa hiyo vitu vinavyotajwa kuwa ni matunda ya miaka 50 ya Uhuru sio zawadi kwa watanzania bali ni wajibu, watanzania kama jamii mojawapo ya wanadamu kosonga mbele ilikuwa lazima. Ndiyo maana mie nasema sio gift wala suprise kama baadhi ya wanasiasa wanavyotakakuliweka suala hili. Haki ni ya kwako wewe unaandaliwa kupiga makofi.

Pili nauliza swali ambalo mie linaninifanya nichefuke, kuwa raslimali tulizonazo na na maendeleo haya ya miaka 50 tunayotaka kusherekea vinaendana/vinalingana au vinakaribiana? Sisi tuna maji ya kutosha mito, Maziwa Tanganyika, Victoria, Nyasa na mengineyo lakini tunapeta na giza, je unasherekea nini? Angalieni migodi tuliyoisikia tangu enzi hizo kama mwadui , na mingine ambayo kwa mujibu wa the "Tanzania National Website" haya ni majigambo:-

Maliasili
Madini – dhahabu, almasi, tanzanite, mawe mengine ya thamani, gesi ya asili, chuma, mkaa wa mawe, maji ya chemchem, nta ya kung'ara, magadi na chumvi. Wanyama na Utalii: Mbuga 12 za wanyama, Eneo la Hifadhi la Ngorongoro, Hifadhi za wanyama 13, Hifadhi maalum za wanyama 38 na sehemu za hifadhi za utamaduni 120.

Uvuvi:Hufanyika kwenye maziwa makuu matatu ambayo ni Victoria, Tanganyika na Nyasa pamoja na mito na pwani ya Bahari ya Hindi. Pato la samaki linaloweza kupatikana kwa mwkaa mzima linakadiriw akuwa tani za metriki 730,000 kwa mwaka, ingawa kwa hivi sasa ni tani 350,000 tu kwa mwaka

Majaliwa ya rasilimali ya madini Almasia, Dhahabu,Metali za besi na kundi la platinamu,Metali za chuma,Bati,Vito,Kaoneti,Makaa ya mawe,Madini ya viwanda. Hapa wamesahau Nikel inayochimbwa huko Ngara maeneo ya Kabanga.

Kabla haya madini na raslimali nyingine hazijaanza kutumika ipasavyo Watanzania walio wengi walisoma bure na hata kupata chakula mashuleni, sasa muda huu kila kwenye madini panachimbwa ,wanyama wanawindwa, watalii wengi, wanafunzi wengi maskini wanakosa mkopo. Mtanzania unasherekea kipi. Mtu anashindwa kutimiza wajibu kisha tunajiandaa kushangilia. Tutashangilia kwa hali tofauti. Wakati wengine wanapiga miayo kwa ajili ya njaa, wengine wanapiga miayo sababu ya shibe. Maana miaka hii 50 wamevuna na wameshiba kwelikweli.Leo hii wauguzi hakuna vijijini, watu wanapoteza maisha, miaka 50 watoto wa shule Watanzania wanaenda shuleni bila viatu, Nyumba za walimu vijijini hata mjini tabuu, maabara hakuna, maji bado shida ila kwenye tovuti ya nchi tunajitapa kuwa tuna raslimali lukuki, maana yake nini? Tulipofika ni wajibu na ilibidi tufike lakini si kwa kiasi kidogo namna hiii. Ndio maana nashindwa nisherekee nini??!!!!

Fedha zilizoko mifukoni kwa watu ambazo ni jasho la watanzania ni nyingi ila sisi tunaleana. Wenye hizo fedha mifukoni wajiandae kusherekea maana wao wamevuna. Na ninaelewa watanzania wachache watakaopewa T-shirt na maji ya kunywa watashangilia lakini wakirudi nyumbani watakutana na giza kama kawaida. Badala ya kujisifu na sifa za kijinga tujiulize. Iweje sisi Watanzania wenye miaka 50 tangu tupate Uhuru bado maskini kiasi hiki wakati tuna raslimali nyingi????!!!!!. Uchumi wa Rwanda uko juu yetu pamoja na matatizo yote yaliyotokea. Sisi rushwa na kulindana tu.
Angalieni kibwagizo kutoka tovuti ya taifa " Umasikini: Takriban asilimia 50 ya idadi ya watu wote nchini wanaishi maisha ya ufukara" hii inatajwa bila aibu wala uoga.

Kilimo ndo siwezi kusema, kila mwaka wakurugenzi na watendaji wa vijiji na kata wana kesi mahakamani kwa kuiba mbolea na mbegu za ruzuku, wizi wa pembejeo kila mwaka, power tiller zinatolewa kisiasa siasa tuuu hakuna mpago halisi kwamba tutaachana na jembe la mkono siku moja.
Madini ndo yananiuma maana hata ripoti ya Bomani kuhusu
"Taarifa fupi ya kamati ya Rais ya kuishauri Serikali kuhusu Usimamizi wa sekta ya madini JuzuuNa. 2"utakutana na maelezo yanayoonesha kuwa wananchi wote wanasikitishwa na hali hii. Nanukuu:-

"Takwimu zinaonyesha kuwa shughuli za uchimbaji mkubwa wa madini zimeongezeka kwa kuanzishwamigodi mikubwa sita mipya ya dhahabu kati ya mwaka 1997- 2007. Vilevile kumekuwa na ongezeko la shughuli za uchimbaji wa madini ya vito kama almasi na tanzanite. Aidha shughuli za uchimbaji madini zimeongezeka kutoka wachimbaji wenyeleseni wapatao 2,000 mwaka 1997 na kufikia takribani wachimbaji 7,000 mwaka 2007.Takwimu pia zinaonyesha mchango wa sekta ya madini umeongezeka kutoka 1.7%mwaka 1997, na kufikia 3.8% mwaka 2006.

Miongoni mwa malalamiko ya wananchi ni pamoja na hali inayoonekana ya sekta ya madini kutochangia vya kutosha katika maendeleo ya nchi hasa ya kiuchumi na kijamii. Pia imeonekana kuwa mikataba ya madini inapendelea zaidi makampuni makubwa ya uwekezaji katika madini, huku kukiwepo na usiri mkubwa wa mikataba hiyo." Kwa taarifa nzima bofya hapa : http://swahili.policyforum-tz.org/files/ripotiyabomani.pdf

Kwa hili la sherehe ya miaka 50 ni sawa na kibarua aliyepewa kupalilia shamba la hatua 20 kisha akapatiwa chai ya maziwa nzito, maji ya kunywa, Chapati na nyama ili afanye kazi vizuri lakini kuanzia asubuhi saa 12 hadi jioni saa 11 alikuwa kapalilia hatua mbili tu!!! Alipoulizwa kulikoni mtu unapewa kila nyenzo ili ufanye kazi vizuri alijibu " kwani sikupalilia?" ukweli ni kuwa alipalilia lakini vitendea kazi alivyopewa na kazi iliyofanyika ni sifa ipi angepewa huyu bwana. Kazi ilikuwa ni moja kumuachisha kibarua huyo na kumtafuta anyefaa.

Hii ni sawa na sisi Watanzania ambao kwa akili zetu tunamg'ang'ania na kumshangilia kibarua huyo mwenye kula mikate, nyama, maziwa na kushiba lakini akapalilia hatua mbili. Na sisi Watanzania tutashangilia kweli siku hiyo. Kibarua anafaaa? Naomba niwasilishe japo kwa uchungu pale Haki ya mtanzania inapogeuzwa kuwa Gift (zawadi) tena yenye Surprise!!!
 
Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
58,561
116,709

Mkuu salute! Umenena maneno na mifano mizito inayodhihirisha kuwa jamii ya Watanzania ni jamii yenye upungufu wa akili ya kuzaliwa ya kujua lipi la kweli na lipi la uongo, Watanzania wengi wako tayari kujisihaulisha shida wanazopata kila kukicha kwa mkate wa siku moja tena hongo hiyo inatolewa na mhusika anayewasababishia shida izo. Wanasiasa wanatumia nguvu kubwa na gharama kubwa kuwafanya watanzania kuwa watumwa wa kufikiri na wanawapata wengi. Watanzania wamesilibwa uongo mpaka hawatambui kuwa hawatendewi haki na watawala wao. Imefikia hatua mpaka masikini wanaoteseka kwa ugumu wa maisha wanahongwa Tsh elfu mbili ili wakazomee kundi flani linapowasilisha hoja ya kuwatetea maskini hao-hao kaitika midahalo mbalimbali inayoendelea hapa Tanzania. Watawala wamesongwa na uchu wa madaraka kwa nia ya kujitajirisha mpaka kufikia hatua ya kununua mashabiki katika shuhuli za kiserikali ili kuwadanganya wananchi kuwa utawala unapendwa na hauna mapungufu ivyo basi, huamasisha wananchi kuacha kudai haki zao kwa kuwaonga elfu mbili mpaka elfu tano kwa kila mwananchi aliyepo eneo husika. Hii miaka 50 ya uhuru inayosherekewa kwa mbwembwe inamaanisha kuwa haya maendeleo kidogo tuliyoyapata ni privilage and not our rights. Tufikirie namna ya kusheherekea hii siku kwa namna yetu ya kipekee mkuu.
 
Ta Muganyizi

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
5,360
2,720
ngoja tuone kama tutafika jamani, sijui kama Watanzania wameliona hili
 
lukindo

JF-Expert Member
Mar 20, 2010
8,470
9,013
Mkuu Daudi, wengi wataona kuwa umeamua kuwatukana Watanzania mchana kweupe lakini hapo kwenye red/underline ni ukweli mwingine ambao wangeueleza katika wakati huu wa miaka 50 ya uhuru. Swali ni je, nanai ataueleza wakati sote tuko hivyo!?
Nimesikia kwenye redio moja asububuhi leo juu ya sala/ibada ya kuiombea nchi, Inasikitisha taifa kuendeshwa kwa maombi na likatumia fedha nyingi kwenye kusherehekea 'failure'!
Mkuu salute! Umenena maneno na mifano mizito inayodhihirisha kuwa jamii ya Watanzania ni jamii yenye upungufu wa akili ya kuzaliwa ya kujua lipi la kweli na lipi la uongo, Watanzania wengi wako tayari kujisihaulisha shida wanazopata kila kukicha kwa mkate wa siku moja tena hongo hiyo inatolewa na mhusika anayewasababishia shida izo. Wanasiasa wanatumia nguvu kubwa na gharama kubwa......
.......
....
 
Ta Muganyizi

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
5,360
2,720
Mkuu Daudi, wengi wataona kuwa umeamua kuwatukana Watanzania mchana kweupe lakini hapo kwenye red/underline ni ukweli mwingine ambao wangeueleza katika wakati huu wa miaka 50 ya uhuru. Swali ni je, nanai ataueleza wakati sote tuko hivyo!?
Nimesikia kwenye redio moja asububuhi leo juu ya sala/ibada ya kuiombea nchi, Inasikitisha taifa kuendeshwa kwa maombi na likatumia fedha nyingi kwenye kusherehekea 'failure'!

Mkuu Lukindo hapo kwenye red ndo na mimi napashangaaaaa, watu wanasherekea kushindwa sijawahi ona tangu nizaliwe.
 
mfianchi

Platinum Member
Jul 1, 2009
11,204
7,051
Watanzania sijui tuna laana ,kuna siku nilikuwa kwenye daladala iendeyo Afrikana,tulipofika pale kwa Komba nikamsikia mama mmoja akisema anshangaa watu wanaosema eti hakuna lolote serikali inalolifanya na eti kuwa haijafanya lolote wakati serikali inajenga barabara kama hii ya Mwenge hadi Tegeta,naam hao ndio Watanzania wanaangalia kujengwa kwa barabara ya Tegeta eti kuwa ndio maendeleo.
 
Ta Muganyizi

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
5,360
2,720
Watanzania sijui tuna laana ,kuna siku nilikuwa kwenye daladala iendeyo Afrikana,tulipofika pale kwa Komba nikamsikia mama mmoja akisema anshangaa watu wanaosema eti hakuna lolote serikali inalolifanya na eti kuwa haijafanya lolote wakati serikali inajenga barabara kama hii ya Mwenge hadi Tegeta,naam hao ndio Watanzania wanaangalia kujengwa kwa barabara ya Tegeta eti kuwa ndio maendeleo.

Ndugu yangu shangaa na wewe sasa tuwasaidieje watu kama hao. Inabidi watu warudi majukwaani kuwahubiri wananchi.
 
Bigirita

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
15,866
7,161
Na kuna mwanasiasa moja mwenye ndugu zake kule gombe na mahale mountains atakuwa anafoka kwenye TV...TBC to be specific kwamba tz was nothing in 1961 na if not for ccm, we would all be living like his uncles kule gombe.
i hate this guy.
T-shirt na maji ya kunywa vitatuweka barabarani kushangilia
 
Ta Muganyizi

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
5,360
2,720
Na kuna mwanasiasa moja mwenye ndugu zake kule gombe na mahale mountains atakuwa anafoka kwenye TV...TBC to be specific kwamba tz was nothing in 1961 na if not for ccm, we would all be living like his uncles kule gombe.
i hate this guy.

Tell the Guy that any society is dynamic. Hayo machache ayaonayo bado kaibiwa aache ujinga.
 
SEAL Team 6

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
655
118
Watanzania ni wavivu wa kusoma, kwakweli hii article na jinsi ilivyoainishwa kwenye hiyo repoti ya Jaji Bomani, kama repoti hiyo itaweza kusomwa na Watanzania wapatao angalau asilimia 40% wananchi wangeingia barabarani siku nyingi sana, lakini Serikali inatumia nguvu kubwa vyombo vyote vya dola kuwakandamiza wananchi wake kuwatia hofu na hata kuwaua ili walinde hao mafisadi.
 
Bora wewe umeliona hilo, hata hiyo article Wana Jf hawajaisoma wanaona ndefu, hebu washauri mkuu.
 
Bigirita

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
15,866
7,161
Tell the Guy that any society is dynamic. Hayo machache ayaonayo bado kaibiwa aache ujinga.
Mkuu, hawataki kuelewa hilo kabisa hawa jamaa.
Its a pit that a few of us have recognized their barbaric tricks....Watajibeba for sure...........in a very very future!!!
 
abduel paul

Senior Member
Nov 23, 2010
133
5
Wana Jf naomba mnisaidie katika mawazo haya...! Hivi kuna utafiti au wathubutu watakao tafiti juu ya hasara na matatizo yaliyotokea tangu kupatikana kwa uhuru? Maana yawezekana tukawa kweli hatuna hata haja ya kujinyima kushangilia tena na kufanya ziwe siku za public holly zapata tatu kwani tumefanikiwa, lakini tumepata muda wa kuangalia yale yaliyo anguka ndani ya miaka 50? Wakati mwingine nilisha wahi kuwaza what if kila kitu kingebaki kama kilivyo kabla ya miaka 50? Je miaka 50 ilo pita palikua na njaa? Life expectancy ilikua hivi? Furaha na raha zilikua hivi? Nk
 
Ndugu ni vigumu binadamu kuangalia alipo acha kinyesi, kawaida huvunga yeye hajakinya. Lakini huangalia pale anaponyooshea nguo na kujipakia mafuta!!!! Serikali hiii tabu tupu?
 
Nyunyu

JF-Expert Member
Mar 9, 2009
4,354
1,005
Watanzania sijui tuna laana ,kuna siku nilikuwa kwenye daladala iendeyo Afrikana,tulipofika pale kwa Komba nikamsikia mama mmoja akisema anshangaa watu wanaosema eti hakuna lolote serikali inalolifanya na eti kuwa haijafanya lolote wakati serikali inajenga barabara kama hii ya Mwenge hadi Tegeta,naam hao ndio Watanzania wanaangalia kujengwa kwa barabara ya Tegeta eti kuwa ndio maendeleo.

mfianchi, usishangae mkuu, maana mtaji wa serikali ya CCM kwa wananchi wake ni umasikini, na katu hatauondoa maana huo ndo unaendelea kuwapa rubber stamp ya kutawala.

Nasema hivyo kwa kuwa huyo mama, hajui kusoma na tena kinge ni shida kwake, kwani finencer wa mradi wa bara bara ya Mwenge -Tegeta ameandikwa kwenye bango hapo mwenge. Ni "walipa kodi wa japan"

Kwa akili yake ni serikali imejenga bara bara hiyo, bara bara ambayo inajengwa kwa sababu tu imetengeneza ajira kwa wajapan, maana toka contractor, sub-contractors na consulatants ni wajapan, so kwa muda wa miaka mitatu ajira imetengenezwa japan kwa msaada hapa kwetu. Ujinga wetu ndo unaendelea kutufanya tusherekee miaka 50 ya uhuru wa nchi isiyokuwepo!!!

Ipo siku yao tu, maana kazi ni nzito, inahitaji wananchi kama huyo mama ulokuwa naye kwenye dala dala ajitambue, ndo tutawafukuza hawa wakoloni weusi.
 
Ta Muganyizi

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
5,360
2,720
Watanzania wana mcheche, utawaona na nguo za kijani wanaimba badala ya kulia kwa kuibiwa miaka 50 yote ya Uhuru
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

4 Reactions
Reply
Top Bottom