Rashid Mamboleo Makoko

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,915
30,259
MAMBOLEO RASHID MAKOKO MWANATANU WA TANGA LONDON YA 1958

Ukitaka kumweleza Rashid Mamboleo Makoko lazima kwanza uanze na baba yake Mzee Makoko Rashid.

Tanga kuna barabara inaitwa Makoko Road hii barabara ni kwa ajili ya heshima na kumbukumbu ya Mzee Makoko katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Barabara hii ni maarufu sana kama walivyo wenyewe ukoo wa Makoko mjini Tanga.

Ni nani huyu Rashid Makoko?

Nitamweleza Mzee Rashid Makoko kama nilivyomwandika katika kitabu cha Abdul Sykes:

''...tarehe 23 Oktoba, 1954 wanachama wa mwanzo wa TANU huko Tanga walikutana kuchagua uongozi wa chama.

Hamisi Heri alichaguliwa kuwa Mwenyekiti na Peter Mhando katibu.

Jumla ya watu 45 walihudhuria mkutano huo na wakapewa kadi za TANU.

Mwalimu Kihere alihudhuria mkutano ule lakini hakuchaguliwa katika nafasi yoyote ya uongozi.

Kamati ya wanachama iliundwa kutokana na wale wanachama kumi na moja waasisi waliokutana katika ule mkutano wa kwanza mwezi uliopita.

Kamati hiyo ilikuwa na wajumbe wafuatao: Abdallah Rashid Sembe, Mohamed Kajembe, Victor Mkello, Dhili Mgunya, Ali Mohamed, Abdallah Mohamed na Mohamed Sadik.

Peter Mhando alijitolea nyumba yake kuwa ofisi ya kwanza ya tawi la TANU mjini Tanga.

Mara tu baada ya mkutano huu wazee wa Tanga wakiongozwa na Makoko Rashid, mwanachama wa zamani wa TAA walianza kufanya kampeni kwa ajili ya TANU.

Chama kilipata msukumo mwingine na kuongezeka nguvu wakati Sadik Ali Patwa Muasia tajiri alipoingia TANU.

Nyerere alipozuru Tanga Mwalimu Kihere alitaka kufanya dhifa nyumbani kwake kwa heshima yake.

Uongozi wa TANU, hususan Hamisi Heri na Mzee Makoko walikataa kumruhusu Nyerere kuhudhuria dhifa hiyo kwa sababu Mwalimu Kihere alikuwa hajaonesha kuiunga mkono TANU.

Nyerere akitambua utu uzima wa Mwalimu Kihere, uzoefu na sifa yake ya uongozi katika African Association, alishauri uongozi wa TANU Tanga usiache fursa ile ipite bure.

Nyerere alitoa hoja kuwa, ilikuwa muhimu kukubali mwaliko wa Mwalimu Kihere na kutumia fursa hiyo kumuomba arudi kwenye harakati kwa kuwa TANU ingefaidika kutokana na uzoefu wake alioupata katika African Association.

Kwa ajili ya nasaa hiyo TANU ilikubali mwaliko wa Mwalimu Kihere na Nyerere alihudhuria dhifa ile nyumbani kwa Mwalimu Kihere pamoja na wanachama wengine.

Mwalimu Kihere alikuwa mwanasiasa wa msimamo wa wastani, alikuwa mbali na msimamo mkali dhidi ya serikali.

Kwa ajili hii Mwalimu Kihere alielewana vizuri na utawala wa kikoloni.

Hii ilikuwa kinyume kabisa na wazalendo wengine kama Mzee Makoko Rashid ambaye kwa miaka mingi alijulikana kwa chuki yake dhidi ya Waingereza.

Inasadikiwa kwamba watu wawili wataingia katika historia kwa chuki zao mahsusi dhidi ya Waingereza, mtu wa kwanza ni Schneider Abdillah Plantan na wa pili ni Mzee Makoko Rashid.

Wote wawili walifungwa gerezani na Waingereza kwa sababu ya misimamo yao dhidi ya serikali ya kikoloni.''

Sasa baada ya kumuona baba yake Mamboleo Rashid Makoko, Mzee Rashid Makoko, turejee kwa mwanae.

Mamboleo Rashid Makoko nimekutananae kwa mara ya kwanza ndani ya Nyaraka za Sykes na kitu kilichonivutia sana ni barua zake alizokuwa anamwandikia Ally Sykes kati ya mwaka wa 1958 alipokuwa yuko Uingereza.

Ally Sykes nilipomuuliza habari za Mamboleo Makoko aliniambia alikuwa rafiki yake kipenzi na ndiye aliyekuwa mpambe wake siku alipokwenda kumuoa mama yetu.

Sikuhitaji maelezo zaidi.

Kitu cha kwanza kilichonivutia kwa Mamboleo Makoko ni ujuzi wake katika lugha ya Kiingereza.

Kitu cha pili kilichokamata fikra zangu ni jinsi alivyokuwa akichambua matukio yote yaliyokuwa yakitokea Tanganyika wakati wa kupigania uhuru.

Katika hili na hapa nasita siwezi kusema yote niliyosoma ni jinsi aliyokuwa anamwandikia Ally Sykes maneno kama vile anatabiri.

Mamboleo Makoko ukisoma barua zake hizi ni kama vile alikuwa akimpa tahadhari rafiki yake na wakati mwingine akimuuliza Ally Sykes nini msimamo wake kwa jinsi mambo yalivyokuwa yanakwenda.

Mamboleo Makoko alikuwa akimgusia Ally kuwa mwangalifu kuhusu hali ya baadae uhuru ukishapatikana.

Sikuweza kuzitumia barua hizi katika kitabu nilichokuwa naandika kwa kuhisi uzito wa yale maneno na kwa sababu nyingine pia.

Lakini nilivutiwa sana na barua hizi hasa siku nilipokutana na barua nyingine kutoka kwa Mangi Mkuu Thomas Marealle akimwandikia Ally Sykes na kumpa tahadhari kama ile niliyosoma katika barua ya Mamboleo Makoko.

Makoko alikuwa na kipaji cha uandishi.

Barua zake kwa Ally Sykes zilikuwa zikianza kwa maskhara kisha ndiyo anaandika kile alichokusudia.

Nilikuwa kila nikikutana na barua ya Makoko nitaifungua na kuisoma.

Barua hizi zote niliamua kuziweka pembeni sitazitia katika kitabu cha Abdul Sykes nikijifariji kwa fikra kuwa mradi hizi nyaraka akina sasa zimefunguliwa kwa ajili ya utafiti watakuja watafiti wengine baada yangu na In Shaa Allah watazipitia barua hizi na wataandika waliyoyaona humo.

Mimi nikajifunga katika kuandika maisha ya Abdul Sykes.

Ally Sykes akanieleza kuwa Watanzania wengi walikuwa wanaanza kufanya biashara pale London baada ya uhuru pamoja na yeye walisaidiwa sana na Makoko na takriban wote walifanikiwa na kutajirika.

Mamboleo Makoko alipofariki David Wakati alitoa wasifu wa Makoko katika kipindi chake maarufu kilichokuwa kinaitwa, ''Nipe Habari.''

Picha ilipigwa katika mgahawa wa Sadiki Patwa Tanga wakiwemo Mwalimu JK Nyerere na Bw. Patwa kulia kwake unapoitazama picha.

Kulia mwenye koti na kofia Mzee Rashid Makoko na wa pili yake ni mwanae Rashid Mamboleo Makoko na kushoto mwenye koti na kofia Mzee Makata Mwinyimtwana tajiri mkubwa Tanga katika miaka ya 1950/60.

Picha nyingine ni Mwalimu Kihere.

1606743763027.png
 

Attachments

  • 1606746723730.png
    1606746723730.png
    58.2 KB · Views: 6
  • 1606746808644.png
    1606746808644.png
    76.6 KB · Views: 5
  • 1606747099473.png
    1606747099473.png
    31.3 KB · Views: 6
Inasisimua sana. Na naujua utamu wa kusoma barua za zaman.kabla ya masimu haya zaman ni barua tu.na posta inafanya kazi.akhi zetu waliokuwa nje miaka hio wanaadika makurasa kwa makurasa. Unasuuzika sana kusoma vitu vya enzi hizo.namna mtu anavomaliza yote kwenye barua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
inasisimua sana.na naujua utamu wa kusoma barua za zaman.kabla ya masimu haya zaman ni barua tu.na posta inafanya kazi.akhi zetu waliokuwa nje miaka hio wanaadika makurasa kwa makurasa.unasuuzika sana kusoma vitu vya enzi hizo.namna mtu anavomaliza yote kwenye barua

Sent using Jamii Forums mobile app
Julai...
Ukimsoma Makoko utastarehe na nafsi yako.
 
Mzee Muhammed Said ni hazina adimu sana kwenye historia ya Tanganyika.
Hivi Mohamed Said huyu ndo wa kwenye kipindi flani cha TBC cha kiswahili miaka ya nyuma?

Nakumbuka kile kipindi maranyingi walikua wakialikwa wakina Mohamed Said,Mudhihir,Abdalla Safari.muongoza kipindi Mzee Suleiman Hega.
 
Mzee Muhammed Said ni hazina adimu sana kwenye historia ya Tanganyika.
Hivi Mohamed Said huyu ndo wa kwenye kipindi flani cha TBC cha kiswahili miaka ya nyuma?
Nakumbuka kile kipindi maranyingi walikua wakialikwa wakina Mohamed Said,Mudhihir,Abdalla Safari.muongoza kipindi Mzee Suleiman Hega.
Nawa...
Hapana ni majina kufanana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom