Rangi za vazi la majaji

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
15,539
19,389
Sina uhakika kama hapa ni mahala pake, ila kwa vile ndiyo sehemu ninayotembelea mara kwa mara, nimeamua kuiweka hapa. Modereta anaweza kuihamishiwa panpahusika.

Nimeangalia kwa makini sana mavazi ya spika na yale ya majaji wetu nikajiuliza swali moja kuhusiana na mbunifu wa mavazi hayo; je aliangalia rangi za bendera ya taifa kwa makini kabla ya kuyabuni mavazi ya majaji wetu?

Rangi ya mavazi hayo haifanani kabisa na rangi za bendera ya Taifa, inabidi uwe makini sana kuangalia ile nembo ya shingoni ndipo ujue kuwa hawa ni majaji wa Tanzania.

Najua kuwa majoho ya majaji yanaweza kuchukua rangi yoyote ila nadhani kuwa tungekuwa systematic zaidi kwa kuhakikisha kuwa rangi za majoho ya majaji wetu zinaashitoa serikali ya Tanzania hasa kwa vile rangi za joho la spika wetu linaonyesha hivyo.
 
kwa vile ndiyo sehemu ninayotembelea mara kwa mara, nimeamua kuiweka hapa
hau make sense, hebu ondoa hiyo talalila hapa, sio mahali pake
 
hau make sense, hebu ondoa hiyo talalila hapa, sio mahali pake
Haja make sense, nilidhani uta-make, lakini huja-make sense hivyo hujanisaidia mimi wala mtoa mada a-make sense hivyo huja-make sense.
 
hau make sense, hebu ondoa hiyo talalila hapa, sio mahali pake

Na hii yako ndo sense! bangi za asubuhi mbaya sana na hasa katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu :focus:
 
Back
Top Bottom