Ranfred masako, wa itv kwanini sikubalini na sensa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ranfred masako, wa itv kwanini sikubalini na sensa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Simba Mkali, Aug 25, 2012.

 1. Simba Mkali

  Simba Mkali JF-Expert Member

  #1
  Aug 25, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 591
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  nalishangaa jitu zima kama Ranfred Masako la ITV kuendelea kutumia kuandaa kipindi kwa ajili ya kuwatukana watu kwa kuwaita wanatumiwa, siyo wazalendo,wajinga na kashfa nyingine nyingi kwa kuwa hawataki kuhesabiwa katika Sensa itakayofanyika kesho nchi nzima.
  Naweza kuonekana kuwa ni Muislamu mwenye itikadi kali lakini upeo mdogo wa Masako na wale aliowaalika katika kipindi chake cha Kipima Joto cha jana ndiyo kilichonifanya kusema haya:
  sikubalini na sensa kwa kuwa zilizotangulia hazikuwa na manufaa yoyote kwa taifa hili. mfano wakati soko la Kariakoo lilipokuwa likijengwa iliachwa nafasi kuanzia soko dogo hadi barabara ya Lumumba kama reserve ya soko lakini walafi wakauza viwanja na kujenga majumba, hapa hapakuhitajika sensa.
  Bado, serikali imewahamisha wafanyabishara kuwapeleka soka la Ilala leo, hii soko limefurika mitaa imejaa uchafu, sensa za miaka 1967, 1977, 1988, 199... 2002 hazikuona kama soko la Ilala lilihitaji kupanuliwa? Pia, ningeweza kuisapoti sensa kama serikali ingekuwa inawajali wananchi wake kwa kufika nje Miji na kupanga plani za viwanja kupeleka umeme na maji kwa ajili ya wananchi wake. lakini yote ni kazi bure, sioni kwanini nihesabiwe kwanza vyeti vya kuzaliwa na vifo vinatolewa kwanini wasihesabu hukohuko? Mi naona ni njia zao za kuendeleza kula tu.
  Namuuliza Masako, kama kweli sensa ina maana kule kwao Mahenge kuna hospitali ngapi, kwanini dawa hakuna hospitali? kwanini wagonjwa wanalala chini muhimbili? acha ujinga.. usiwe kama babu jinga mali zako zinaliwa huku unaangalia, kaa hapo ITV ulipwe posho zako na Mengi ukalale.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Aug 25, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Broda mbona na wewe tena una jazba na tunashindwa kuwatofautisha?
  Point zako ziko sawa, lakini unaweza kunijibu iwapo sensa hazijaleta maendeleo nchini kwanini liwe suala la Waislamu na si Watanzania?

  Lakini pia hoja yako kuwa watu wa sensa wahesabu vyeti vya uzazi na vifo ni ya Mtanzania aliyezaliwa Ulaya na amekua na anazeekea huko!
  Kwa mtu wa kawaida hawezi kutamka hoja hiyo maana asilimia 70 ya watz wanajifungulia mashambani!
   
 3. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #3
  Aug 25, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Dah,,,,hahahahaaaa,,,,,,,nimebaki gaaa kama mchuz wa dagaaa,,,,MASAKO UNALO HILO,
   
 4. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #4
  Aug 25, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  pj,,,,,nipe tofauti za hapo juu,halafu tuendelee na mjadala,na unambie wewe upo kundi gani,la waislam au watanzania
   
 5. Simba Mkali

  Simba Mkali JF-Expert Member

  #5
  Aug 25, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 591
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Tofauti yangu na Masako ni kubwa sana, miye ninajielewa yeye jhajielewi. Hivi hizo balozi zetu zinafanya nini huko nje kama hazijui idadi ya watanzania wanazaliwa na wanakufa huko nje ni heri zifungwe zitakuwa hazina maana hata kidogo. Mmarekani akifa bongo kwao wanajua au kwa kuwa siye ni watoto wa mbwa? Yaa nakubaliana na wewe kwamba lilitakiwa suala la Watz kusimama kidete kuipinga sensa kwa kuwa inakula fedha zetu, hivi bilioni ngapi zinateketea wakati tunakosa vitu vya msingi?
   
 6. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #6
  Aug 25, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Vileee vileee aliyasema hayooo katika mkutano wa kimataifaaa uliofanyika katika ukumbi wa aicc,nikilipoti kutoka arusha ni mimi rainfred masako wa ITV.
   
 7. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #7
  Aug 25, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,333
  Likes Received: 2,641
  Trophy Points: 280
  Aisee kumbe alitukana sana eenhh!
  anyway mkuu mleta mada,tambua tu serikali yetu inayojiita sikivu haijitambui, wameanza madaktari wakajitutumua yakaisha,wakaja waalimu then inakuja ishu ya sensa.
   
 8. mnyanyaswaji

  mnyanyaswaji JF-Expert Member

  #8
  Aug 25, 2012
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 469
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Yani jana ilikuwa kichefuchefu, kuna yule sijui profesa maji mafupi makengeze anaongea kama anaishi shimoni, eti itajulikana idadi ya pembejeo ngapi etc. Waanze tu kununua vifaaa vya maendeleo wataiba saa ngapi?? Labda sio bongo. Na huyo Masoko sijui nina mashaka na elimu yake pumba tupu.
   
Loading...