Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,245
- 122,342
Heri ya 2017 JF massive.
Dakika chache tu zilizopita kuna jambo jema/ zuri limenitokea.
Nimeamka na njaa ikabidi niwashe gari niende Bojangles kununua staftahi.
Kufika hapo nikaamua kutokushuka kwenye gari hivyo nikatumia drive-thru window.
Nika place order yangu kwenye ubao wa menu. Sasa mbele yangu alikuwepo mtu mwingine kwenye gari lake aliyekuwa anachukua na kulipia order yake hapo dirishani.
Alipomaliza na kuondoka nami nikasogea hapo dirishani ili kulipia na kuchukua nilichoagiza.
Ile natoa debit card yangu kulipia yule mhudumu wa hapo dirishani akanambia kuwa yule mtu aliyekuwepo mbele yangu keshalipia hiyo order yangu. Hivyo akanikabidhi tu hicho nilichoagiza.
Nikapigwa na butwaa la furaha. Furaha si kwa sababu ya kusevu hela ambayo ningetumia bali furaha ya kile kitendo cha yule mtu ambaye simjui na yeye hanijui.
Mtu mwenyewe hata sikumwona anafananaje maana nilikuwa busy na simu yangu nikibishana na limtu huku JF.
Hicho kitendo chake kimenigusa sana. Na kusema ukweli si mara ya kwanza hilo jambo kunitokea. Limeshanitokea mara kadhaa huko siku za nyuma.
Ukarimu wa huyo mtu ambaye hata simjui umenipa hamasa nami nitende jambo kama hilo kwa mtu nisiyemjua. Sijui nitafanya lini na wapi lakini nami nitamlipia mtu order yake hivi karibuni bila hata ya yeye kujua.
Nitafanya hivyo kimya kimya na kusepa ili nami nimjaze mtu furaha hata kama ni kwa muda mfupi maana huwezi kujua hiyo furaha inaweza kuwa na athari gani kwa mtu.
Mtu anaweza akawa anapitia mengi na kitendo kama hicho chaweza kabisa kurudisha matumaini endapo mtu huyo atakuwa amekata tamaa kwenye jambo lolote lile linalomsibu.
Kwa kweli watu wema wapo hapa duniani. Na kilichonitokea mimi leo hii ni ithibati tosha kabisa.
Natamani sana walau ningepata hata sekunde moja ya kumshukuru huyo mtu lakini naamini mwenyewe wala hakutaka hayo. Katenda jambo la wema na akasepa zake.
Wooooow!!
Nothing is more touching than the kindness of total strangers!
Now I'm on my way to do that mannequin challenge but I'm also definitely going to do a random act of kindness to someone.
Hicho ndo nilichoagiza! Nothing major. Just a simple steak biscuit.