Ramadan imenitesa Zanzibar, nimeshindia tende

Ramadan imenitesa Zanzibar, nimeshindia tende

Mkuu
Wakati wa mfungo kisiwani Zanzibar wanakataza kupikwa chakula kwenye migahawa na kula hadharani.Sitaki kuamini kwamba wewe hata nyumbani ulikuwa unashindwa kujipikia au mkeo akakupikia ukala. Mimi nina jamaa zangu wakristo wengi tu ambao walikuwa Zanzibar wamerudi majuzi na walikuwa wanajilia zao mahali walipofikia.Ila wewe unataka kuwaaminisha watu kwamba hukuwa na access ya kula wakati access unayo.
Kikubwa kama wataka kula,kula kwa staha. Mazingira ya Zanzibar na bara ni tofauti has kipindi cha mfungo.

Ushauri wangu:Tujaribu kujifunza tamaduni tofauti za jamii zetu ili tuweze kuendana na mazingira husika,na kama unaona huwezi kuendana na utaratibu wa jamii husika busara ni kuangalia ustaarabu mwingine. Kila jamii ina tamaduni na taratibu zake katika mazingira tofauti.
Mkuu, zanzibar sio kwetu, wala sijapanga zanzibar.
Nilienda kikazi, kwa muda wa wiki moja.

Siijui machimbo ya kwenda kula kwa kujificha. Hata hivyo nisingeweza kwasababu kazi iliyotupeleka isinge niruhusu kufanya hivyo.

Mimi na jamaa zangu tumeshindia tende, maji, na soda.

Mchana tulikuwa tunabeba kwenye begi na kulia kwenye gari yetu. Dereva alikuwa mtu wa kule, hata yeye alikuwa anatushangaa ila akatuzoea.
 
Back
Top Bottom