Rally Bwalya Simba wamepigwa mchana kweupe!

Christopher Wallace

JF-Expert Member
Dec 8, 2015
1,397
3,489
Kwa msimu wa pili mfululizo Simba Sc wanasajili mchezaji idara ya Kiungo kwaajili ya mechi za kimataifa halafu anakuwa galasa!

Wote ni mashahidi mnamkumbuka yule Msudan Sharif El Din "Mhogo Mchungu" alivyokuja kuwa flop. Sasa ni zamu ya kiungo wa Kizambia, Rally Bwalya nae alikuja kwa mbwembwe nyingi ila ameishia kuwa flop. Hajakidhi yale matarajio makubwa ya wapenda kandanda!

Klabu ya Simba ifike wakati wabadilike, badala ya kusajili magarasabya kigeni kwa bei nyingi ni heri wawape nafasi wazawa tu! Huwezi ukamnunua mchezaji kwa bei kubwa halafu mechi kama ya juzi ya Plateau anawekwa benchi na mchezaji mzawa kama Mzamiru Yassin!

Ni hayo tu, povu ruksa!
 
Tatizo wala sio Rally Bwalya.
Shida ni mfumo wa kocha. Tumeshuhudia jinsi Erasto Nyoni alivyokalishwa benchi na huyu kocha, Baada ya Nyoni kufanya vizuri kwenye timu ya Taifa ndio kocha kaumbuka na kuanza kumpa nafasi.

Wapo wachezaji wengine wanaoharibiwa kiwango chao na huyu kocha mfano Kahata, Gadiel na Kagere sio wabovu lakini kocha anakaribia kuua vipaji vyao.
 
Langu si POVU kwani si was msimbazi ila mpenda mpira na AFYA ya soka letu la bongo....

Mkuu huyu Bwalya alikuwa Power Dynamos kwa miaka 5 hivi....amecheza kwa mafanikio sana pale....

Huyu bwana alikataa OFA mbili moto kutoka NKANA FC na ZESCO na kuamua kutoka nje na kuja SIMBA unalijua hilo?!!!

Huyu bwana nimemfuatilia uchezaji wake kule kwao..yuko BOMBA SANA...bado ni mdogo hazidi 26...amekuja ligi ya nje(mpya kwake).

Chama Clatous alipokuja SIMBA haikuwa hii ya SASA....ninyi was mikia sasa mna PRESSURE KUBWA...wachezaji wengi wazuri...viungo wa kumwaga....kufikia mpaka kocha kuona anahitaji one CF mmoja kule mbele...yote ni utajiri wake wa VIUNGO.......

Umemsemea Mzamiru...kumbuka yeye yupo kikosini kwa muda mrefu sasa....mbona hushangai kutochezeshwa KAHATA hata kama si BOX TO BOX MIDFIELDER kama huyu LARRY BWALYA?!!!

Larry has precious things on his feets...give him an enormous time so as you can start to judge his potentials mpwaa...

Sisi Jangwani tunakuja KIVINGINE...

Unauona moto wa TUISILA KISINDA?!!! 🤣🤣
Muulize ONYANGO atakueleza......🤣
 
Tatizo wala sio Rally Bwalya.
Shida ni mfumo wa kocha. Tumeshuhudia jinsi Erasto Nyoni alivyokalishwa benchi na huyu kocha, Baada ya Nyoni kufanya vizuri kwenye timu ya Taifa ndio kocha kaumbuka na kuanza kumpa nafasi.

Wapo wachezaji wengine wanaoharibiwa kiwango chao na huyu kocha mfano Kahata, Gadiel na Kagere sio wabovu lakini kocha anakaribia kuua vipaji vyao.
Ungekuwa we kocha ungemtoa nani acheze Gadiel?!
 
Usajili wa Simba huwa na lengo la kuikomoa Yanga siyo kutimiza mahitaji ya timu yao. Walisikia nia ya Yanga kumtaka Bwalya. Wakawahi wao. Haya sasa wamtumie.
Halafu viongozi qa Mikia wanajisahaulisha kwamba wachezaji wao wazawa ni mabingwa wa misumari.
 
Tokea mwanzo nilijua Bwalya ni mchezaji wa kawaida sana. Mipira ya nguvu haiwezi na hana pasi za mwisho zenye madhara.
ana pasi ndefu za maana sana anapiga long balls vizuri,mechi na jkt kule dodoma uliona simba inavyotakiwa kuwa ikiwa na strikers wawili ile mechi ndiyo simba ninayoijua mimi baada ya hapo UKICHANGANYA MISUMARI +UJINGA W AKISHINGO=sielewielewi yanayoendelea
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom