Edo Kumwembe: Aliyemsajili Sawadogo Simba pepo ataisikia tu

Oldmantz

JF-Expert Member
Jan 24, 2023
430
998
WAKATI Simba ilionekana kama imekosea kuwasajili Victor Akpan na Nassor Kapama katika dirisha kubwa lililopita la uhamisho, hatimaye Januari ikafika. Mtu mmoja mwenye busara zake akaishauri Simba iongeze mchezaji wa kiungo baada ya Akpan na Kapama kuonekana hawafahi.

Mtu huyo akawasiliana na wakala wa mchezaji anayeitwa Ismael Sawadogo. Simba wakahaha kuinasa saini yake. Wakaipata saini yake. Tukatangaziwa kwamba Simba imefanikiwa kuinasa saini ya mkata umeme hodari wa Burkina Faso, Ahmed Ismael Sawadogo.

Wambea tulienda kuchimba mitandaoni kujaribu kutazama timu ambayo alikuwa amechezea tukaona mara ya mwisho alikuwa amecheza soka mwaka mmoja uliopita. Ajabu iliyoje. Ndio alikuwa Morocco mwaka mmoja uliopita na baada ya hapo hakuonekana popote. Aliyetoa wazo la kumchukua hakujua hili?

Kitu kibaya zaidi ni kwamba Simba walikuwa wametoka katika hasara kubwa ya kuilipa Coastal Union shilingi milioni 100 kwa ajili ya kupata huduma za Akpan. Hii ni achilia mbali pesa ambazo walimpa Akpan mwenyewe. Hii ina maana Simba walikuwa wamepata hasara kubwa na hawakupaswa kurudia kosa jingine kirahisi.

Walipaswa kuwa makini. Mtu ambaye alitoa wazo la kumchukua Sawadogo alipaswa kuwa makini zaidi. Ni ukweli kwamba kusajili mchezaji ni jambo la bahati nasibu lakini kwa hapa Simba haikupaswa kufanya jambo la bahati nasibu. Walipaswa kufanya jambo la uhakika zaidi kwa sababu walikuwa wanajipeleka katika msimu mgumu.

Kudorora kwa Jonas Mkude kulimaanisha kwamba mzigo mkubwa ulikuwa unawaangukia Sadio Kanoute na Mzamiru Yassin. Alihitajika mchezaji ambaye angeingia moja kwa moja katika timu na sio kwenda kukaa jukwaani na Mkude. Kwanini asajiliwe Sawadogo? Kwanini asajiliwe mchezaji ambaye hawakuwa na uhakika naye?

Wakati Simba wakihangaika na mchezaji ambaye hawakuwa na.uhakika naye, watani zao walivuka maji kwenda Zanzibar kumchukua kiungo Mudathir Yahaya ambaye alikuwa anakula pweza forodhani huku akiwa hana timu ya kuchezea. Kwanini Simba haikwenda kwa Mudathir? Aliingia Yanga moja kwa moja na amekuwa mchezaji muhimu katika kikosi chao.

Lakini usajili wa Sawadogo ulikuwa unamaanisha kwamba Simba walikuwa wameingia hasara nyingine ndani ya msimu mmoja. Au tunaweza kusema kwamba walikuwa wameingia hasara nyingi ndani ya miezi sita tu. Walikuwa wamekosea kwa Akpan na Kapama halafu wakaja kukosea kwa Sawadogo.

Hatimaye wamempa mkono wa kwaheri Sawadogo. Juzi wametunyemelea wakati wa chakula cha mchana tukaona katika mtandao wameandika 'Thank You Sawadogo'. Kila mtu alikuwa anashangaa kuona kwanini Sawadogo alikuwa anacheleweshwa. Ukweli ni kwamba walikuwa wanapambana naye katika habari ya malipo.

Lazima malipo yake yalikuwa makubwa kwa sababu kuvunja mkataba wa miaka miwili ndani ya miezi sita sio jambo rahisi. Wenzetu pia wanazijua haki zao. Hauwezi kuwapelekesha. Achilia mbali pesa alizopewa wakati anatia saini mkataba wa Simba, lakini amevuna pesa nyingine za kuvunjiwa mkataba wake. Hajaondoka kinyonge. Lazima akaunti yake itakuwa imetuna.

Kuondoka kwake pia kunadhihirisha namna ambavyo Simba imekuwa ikikosea kunasa mastaa ndani ya misimu hii miwili. Sijui nani anayetoa wazo la kunasa mastaa hawa. Karibu mastaa wote waliowasili katika dirisha kubwa lililopita wameachwa. Waliongozwa na Augustine Okrah ambaye binafsi naamini Simba hawakukosea kumsajili kwa sababu alikuwa na kipaji kikubwa. Tatizo ilikuwa nidhamu yake mwenyewe.

Hapa katika kiungo cha chini sijui nani amekuwa akitoa wazo la kunasa viungo. Zamani alikuwa anapatia. Simba imewahi kuwa imara chini ya Fraga halafu baadaye Thadeo Lwanga. Hata kwa Sadio Kanoute walipatia. Tatizo limekuja baada ya Kanoute. Kila anayechukuliwa amekuwa garasa.

Jambo hili linawaweka Simba katika wakati mgumu wa kusajili wachezaji wazuri kwa sababu inatumia kiasi kikubwa cha pesa kuvunja mikataba ya mastaa. Naamini wanaweza kutumia hata zaidi ya shilingi milioni 300 kwa ajili tu ya kuvunja mikataba. Hapo bado hawajaanza kununua wachezaji wapya kwa ajili ya kuimarisha kikosi chao.

Hasara hii sio ya pesa tu. Kukosea kununua mastaa kumesababisha Simba iwe na kikosi finyu. Kikosi chao ni kile kile tu. Kinatabirika. First Eleven yao imeendelea kuwa ile ile tu huku ikiwaacha na benchi dhaifu. Ni tofauti na watani wao ambao wametumia idadi kubwa ya wachezaji kwa sababu wachezaji wao walio ndani na walio nje ya uwanja hawatofautiani sana viwango.

Na sasa umewadia wakati wa Simba kusajili wachezaji mastaa. Wana muda. Dirisha limefunguliwa. Wasifanye makosa ambayo wamekuwa wakiyafanya katika madirisha mawili yaliyopita. Walipatia kwa wachezaji wachache tu kama Kanoute na Henock Inonga. Simba inahitaji kuleta wachezaji ambao watakuja kuwapumzisha akina Clatous Chama.

Watani wao wana wachezaji wawili tu ambao ni muhimu zaidi. Fiston Kalala Mayele na Djigui Diarra. Vinginevyo katika maeneo mengine wana wachezaji bora wamekaribiana viwango. Simba inaweza kwenda bila ya Chama, Shomari Kapombe, Mohammed Hussein 'Tshabalala', Inonga, Chama na Aishi Manula?

Vinahitajika vyuma ambavyo vitakuja kuingia kikosi cha kwanza. Wachezaji wote walioachwa na Simba dirisha hili hawajafikisha hata idadi ya mechi kumi za Ligi kuu. Ina maana walistahili kuachwa. Walikuwa wanakula mishahara ya bure na kusindikiza kundi la wachezaji wachache ambao waliipambania timu zaidi.

Unapokosea kwa Kapama, kisha ukakosea kwa Akpan halafu likaja dirisha dogo la uhamisho la kurekebisha makosa na bado ukamleta Sawadogo tunapata hisia kwamba huenda makosa kama yakaendelea hata katika nyakati muhimu kama hizi.

Sijui kuna kitu gani kimebadilika Simba lakini ukweli ni kwamba kuna wakati walipatia zaidi kusajili na kujikuta wakiwa na kikosi imara chenye machaguo mengi. Kwa sasa wana first eleven imara tu. Lakini ukweli ni kwamba kuna mambo ambayo yanawaumiza zaidi Wanasimba kwa sasa.

Mfano wanavyosimangwa kwamba bila ya Chama timu yao inakuwa si lolote si chochote. Viongozi inabidi walete watu wa kariba yake ili kupunguza umuhimu wake. Ni kama kwa watani zao ambapo kuna wachezaji wengi muhimu lakini maisha yao yanaweza kwenda bila ya hao.

CREDIT: MWANASPOTI
 
Yameshapita hayo, Sawadogo ameondoka na nafasi yake imeshajazwa na Fabrice Ngoma
 
Mtu mmoja mwenye busara zake akaishauri Simba iongeze mchezaji wa kiungo baada ya Akpan na Kapama kuonekana hawafahi.

Mtu huyo akawasiliana na wakala wa mchezaji anayeitwa Ismael Sawadogo.

CREDIT: MWANASPOTI
Hizi ni fitna na shutuma dhidi ya mtu ambaye yeye anamjua ila anaogopa kumtaja. Kwa nini anachukulia mtu anayeshauri mchezaji wa kuziba nafasi fulani aongezwe ndiyo mtu huyo huyo ambaye ameenda kuwasiliana na wakala wakati taratibu za kawaida za usajili wa wachezaji katika timu haziko hivyo?
 
Hutakiwi kufikira sana kwamba kuna maviongozi wapumbavu. Kama jamii tunayoishi imejaa watu wajinga utoe wapi viongozi wenye akili?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom