Raisi wangu Kikwete ni wakati wako kuamka na kuchukua hatua dhidi ya wabunge wako CCM

Mabewa

Senior Member
Oct 30, 2011
128
17
Rais na mwenyekiti wa ccm taifa ndg Jakaya Kikwete huu ni wakati wako wa kuchukua hatua dhidi ya wabunge wa chama chako kwa kukataa kukutana na wewe.
Sababu wanayotoa eti umekataa kuwaunga mkono ktk posho wanayolilia ya 200000/= na UMEWADHARAU KWA KUPELEKA MUSWADA WA MAREKEBISHO YA SHERIA YA KUANZISHA KATIBA MPYA.
Tunaamini uliyafanya haya kwa maslahi ya Taifa lako.
Lakini wabunge wako vilaza hawataki kukubaliana wewe na wamepanga kukukwamisha katika mipango yako.
Sasa sisi wananchi tunakuunga mkono chukua hatua wananchi na wapinzani wako nyuma yako.
Nawasilisha. wa
 
Thubutu.! Kama anaubavu huo, wala hatasema chochote, wala haoni kama ni tatizo.! Kama kawa ataipotezea juu kwa juu hadi itasahaulika, Nani asiyemjua kikwete.! Labda wabunge wapige mkwara wa kutokuwa na imani nae (kitu ambacho hawawezi kuthubutu kufanya)
 
Mchemsho tunamjua rais wetu vizuri huwa anatumia watu kumjibia sasa tumwambie atoke nje aseme mwenyewe.
 
Atawachukulia hatua gani?
Umesahau kama wabunge hao miongoni mwao yumo A. Chenge?
Katika hili mnamuonea tu mzee wa watu, unadhani yeye hapendi kibarua chake?
Thubutu...!!!!!!
 
Kweli kaka hivi hata chenge anathubutu kusema juu ya kikwete?lakini mzee wangu kayataka angewaondoa mapema yasingemkuta au wanamjua sana?
 
Wewe rais wako ni Satta au JK, kama ni JK unapoteza muda wako kumshauri. Acha wafu wawazike wafu wao, wampigie tu kura ya kutokuwa na imani nae, hata kama sababu zao ni posho lakini watakuwa wametusaidia na sisi maana hata sisi katuchosha na hatuna imani nae tena.
 
wakina Sendeka mapovu yanawatoka sijajuwa wanatetea maslahi ya nani?
 
JK ajitokeze hadharani aseme kuwa hayo marekebisho ni ya msingi kwa manufaa ya taifakisha awaambie wanaccm wenzake kupitisha au kutopitisha ni juu yao na hata wakitaka wampigie kura ya kutokuwa na imani naye..yeye anawe mikono. Huo ndio ushauri wangu kwa mh. Raisi. Mungu ampe hekima kuu majira haya.
 
Wewe rais wako ni Satta au JK, kama ni JK unapoteza muda wako kumshauri. Acha wafu wawazike wafu wao, wampigie tu kura ya kutokuwa na imani nae, hata kama sababu zao ni posho lakini watakuwa wametusaidia na sisi maana hata sisi katuchosha na hatuna imani nae tena.

Kapotolo uyasemayo ni sahihi sema katika hili hebu tuache itikadi na tumtetee kwa maslahi ya Taifa zima mana yote wanayomtuhumu nayo ni juu ya maslahi ya Taifa wala si maslahi yake.
 
Ha ha ha ha ha! Ikiwezekana kuwe na makubaliano rasmi kati ya Kikwete na wapinzani kwamba endapo upinzani utachukua nchi Kikwete na familia yake hawatashtakiwa kwa makosa yoyote (kama yapo) ambayo waliyafanya siku za nyuma. Naamini kwa njia hii Rais atakuwa na confidence ya kupambana na haya majuha mabunge ya CCM yasiyojua kilichoyapeleka Bungeni.

Hopefully, issue hii (ya kutomshtaki Rais na familia yake) ni kati ya mambo CHADEMA mliyogusia wakati wa mazungumzo na Rais Ikulu hivi karibuni.
 
JK ajitokeze hadharani aseme kuwa hayo marekebisho ni ya msingi kwa manufaa ya taifakisha awaambie wanaccm wenzake kupitisha au kutopitisha ni juu yao na hata wakitaka wampigie kura ya kutokuwa na imani naye..yeye anawe mikono. Huo ndio ushauri wangu kwa mh. Raisi. Mungu ampe hekima kuu majira haya.

Kiukweli kabisa...upo sahihi asilimia 100
 
Mungu aliiangamiza sodoma na gomora kwa kukosekana hata mtu mmoja wa kutubu,sasa chama changu kinaelekea kufa kama hatapatikana mwerevu mmoja tu kukiokoa.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Wewe rais wako ni Satta au JK, kama ni JK unapoteza muda wako kumshauri. Acha wafu wawazike wafu wao, wampigie tu kura ya kutokuwa na imani nae, hata kama sababu zao ni posho lakini watakuwa wametusaidia na sisi maana hata sisi katuchosha na hatuna imani nae tena.

Du wakifanya kitu kama hicho watakuwa wamechangia kuikomboa Tz kwa kiasi kikubwa sana
 
JK ajitokeze hadharani aseme kuwa hayo marekebisho ni ya msingi kwa manufaa ya taifakisha awaambie wanaccm wenzake kupitisha au kutopitisha ni juu yao na hata wakitaka wampigie kura ya kutokuwa na imani naye..yeye anawe mikono. Huo ndio ushauri wangu kwa mh. Raisi. Mungu ampe hekima kuu majira haya.

Kwani yeye si hayupo teyari kupoteza ajira yake?
 
Mungu aliiangamiza sodoma na gomora kwa kukosekana hata mtu mmoja wa kutubu,sasa chama changu kinaelekea kufa kama hatapatikana mwerevu mmoja tu kukiokoa.MUNGU IBARIKI TANZANIA.

Nikuakikishie mkuu hakuna hata mmoja wa kutubu maana wanachukulia kutubu ni kukihasi chama chao kilichojijita kwenye maovu
 
Back
Top Bottom