My friend kwa matukio niliyo yaona kwenye chaguzi za ccm. huyu jamaa anaweza chukua nchi so softly.
Kwa mazingira ya Tanzania ya leo sidhani ni rahisi kama unavyofikiria mkuu,watu wako makini kuliko mtu anaweza kuelezea.Mimi sielewi vizuri kama Mh.Lowasa keshapitishwa na Chama chake kupeperusha bendera kwa nafasi ya urais ambayo haijatangazwa popote,naweza kudhani kuwa anayo nia.Sasa kama hivyo ndivyo bado siamini kama mtu akipitishwa na chama chake basi amechukua nchi kiulaini,sitaki kuamini urahisi huo upo Tz na kwa mazingira ya kisiasa kwa sasa.Labda unisaidie chama cha mapinduzi kina wapiga kura waaminifu wangapi?na vyama vingine pia vinawapiga kura waaminifu kwa vyama vyao wangapi then wangapi hawatabiriki inaweza kuwa sehemu nyingine ya kuanzia vinginevyo nadhani safari ni ndefu na ngumu sana.Labda wewe mkuu unatumia vigezo gani vya kumkabidhi Mh.Lowasa Madaraka ya urais sasa?My friend kwa matukio niliyo yaona kwenye chaguzi za ccm. huyu jamaa anaweza chukua nchi so softly.