RAisi ajaye atauza nini sasa?

RAisi ajaye atauza nini sasa?

Magulumangu

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2010
Posts
3,051
Reaction score
462
Jamani wanajamvi tangu nchi yetu Tanzania ipate uhuru ni maraisi wanne sasa tunao kuna mengi ya kujiuliza nini tumepata na nini tumekosa katika ngwe zote nne za marais wetu,sina kumbukumbu nzuri sana lakini navyojua mie(if am wrong nisahihishwe)

NYERERE(MCHONGA)
Sijui kama kuna shutuma ya kuuza vitu vyetu ila najua kuhusu uhujumu wa umma ambapo watu kibao walilizwa mali zao na kuwekwa nyuma ya NONDO...

MWINYI(RUKSA)
Huyu alishirikiana na mke wake mdogo(bibi sitie) kulamba mbuga na wanyama wetu na kuuza huko uarabuni,mzee wa kuachia tu kwa bibie bila kujali wabongo(mie sitaji mazuri yao)

MKAPA(THe Biggie)

Huyu nae kalamba sana mpaka kala na mzinga,EPA,hapo makaa ya mawe pia alishirikiana na mamaa kuimaliza nchi yetu..

KIKWETE(TOZI Wa IKULU)

hapa hata chichemi wazee wenyewe mnayajua yanayoendelea hadi leo, Kigamboni kailamba pia na hapa Swali ni moja tu,je,nani yuko tayari kutujengea TANZANIA mji wa kisasa kuliko miji yote duniani je hao hawapendi kujenga nchini kwao kuwe kwa kwanza,maana mie hainiingii mkichwa wakuu..

NEXT PREZIDA

Swali langu linakuja hapa,huyu next presidaa atauza nini jamani maana vya kuuzwa naona kama vimepungua au mnaonaje...Tukaeni macho wakuu tutauzwa na sisi sasa maana hakuna cha kuuza...

NEXT FIRST LADY...

Mama Nyere hakuwa na NGO au ni mambo ya zamani hayo jamani?huyo next atakuja na nini?maana Salma kaacha kazi(profesional yake) ya kufundisha na kuanzisha WAMAZA sijui?

Liinchi litauzwa sasa wazee...
 
Back
Top Bottom