Rais Zelensky azilaumu nchi za Magharibi kwa woga

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,005
9,872
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky amezishutumu nchi za Magharibi kwa woga, wakati ambapo nchi yake inapambana kuzuia uvamizi wa Urusi.

Akilihutubia taifa jana usiku baada ya Rais wa Marekani, Joe Biden kusema hataki mabadiliko ya utawala Urusi, Zelensky amekemea kigeugeu cha nchi za Magahribi kuhusu nani na jinsi gani akabidhi ndege na silaha nyingine, huku mashambulizi ya makombora ya Urusi yakiwaua raia.

Zelensky ameomba kupewa ndege za kivita na vifaru ili aweze kujilinda kutokana na uvamizi wa Urusi. Kiongozi huyo wa Ukraine amesema nchi za Magharibi zinahitaji ujasiri zaidi katika kuisaidia Ukraine kupambana na Urusi.

Wakati huo huo, Zelensky amesema vipaumbele vyake vitakuwa uhuru na uadilifu wa eneo hilo katika duru ijayo ya mazungumzo na Urusi. Amesema uhakikisho madhubuti wa usalama ni wa lazima.

Zelensky pia amewaonya raia wa Ukraine kuhusu hatari ya kushirikiana na Urusi.

DW Swahili
 
Alidhani Ni utani.
FOj6Qf1VgAE1wB3.jpg
 
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky amezishutumu nchi za Magharibi kwa woga, wakati ambapo nchi yake inapambana kuzuia uvamizi wa Urusi. Akilihutubia taifa jana usiku baada ya Rais wa Marekani, Joe Biden kusema hataki mabadiliko ya utawala Urusi, Zelensky amekemea kigeugeu cha nchi za Magahribi kuhusu nani na jinsi gani akabidhi ndege na silaha nyingine, huku mashambulizi ya makombora ya Urusi yakiwaua raia. Zelensky ameomba kupewa ndege za kivita na vifaru ili aweze kujilinda kutokana na uvamizi wa Urusi. Kiongozi huyo wa Ukraine amesema nchi za Magharibi zinahitaji ujasiri zaidi katika kuisaidia Ukraine kupambana na Urusi. Wakati huo huo, Zelensky amesema vipaumbele vyake vitakuwa uhuru na uadilifu wa eneo hilo katika duru ijayo ya mazungumzo na Urusi. Amesema uhakikisho madhubuti wa usalama ni wa lazima. Zelensky pia amewaonya raia wa Ukraine kuhusu hatari ya kushirikiana na Urusi.

DW Swahili
Zionist scumbag
IMG_20220326_191816.jpeg
 
..."Akilihutubia taifa jana usiku baada ya Rais wa Marekani, Joe Biden kusema hataki mabadiliko ya utawala Urusi"..
_______---------_________--------_______--------_____

Point of correction***

Senile joe BIDEN karopoka wazi kuwa Putin hafai kubaki madarakani, matamshi ambayo White House waneyamekanusha kuwa sio mpango wa Marekani.

Ila kwa mtu mwenye akili timamu, hawezi kuyapuuzia.
 
Mbona Vita ameshinda??
Kila siku wanaua wanajeshi wa Kirusi 30,000
Wanatungua fighter jets, helicopter, wanapiga kombora meli za kivita,
Wanatutangazia jinsi Ukraine anavyomchakaza Mrusi!

Lawama za nini tena wajameni!??

President Zelensky please! U r winning the war, relax, Ur friends are supplying you with all military equipments & commandoes😆😁

Jinga wahedi huyo!
 
Amechimba mwenyewe aingie mwenyewe.

Biden kashajizeekea wala hakumbuki kama alikwenda Poland.
Hahahahahahahaha hahahahahahahaha hahahahahahahaha hahahahahahahaha haha......! Nimecheka kwa sauti!

Wanasema usimpe lifti shetani! Siku zote atataka kuendesha tu! Atakapokama uskani unafikiri ni wapi atakupeleka kama si upotevuni? Zele alijichanganya sana kuchezea sharubu za Urusi!
 
Mbona Vita ameshinda??
Kila siku wanaua wanajeshi wa Kirusi 30,000
Wanatungua fighter jets, helicopter, wanapiga kombora meli za kivita,
Wanatutangazia jinsi Ukraine anavyomchakaza Mrusi!

Lawama za nini tena wajameni!??

President Zelensky please! U r winning the war, relax, Ur friends are supplying you with all military equipments & commandoes😆😁

Jinga wahedi huyo!
Ahaaaaa propaganda za magharibi,putin is going well with his plan
 
Ni kawaida kwa west kumtumia mtu kisha kumtupa. Saddam Hussein aliwahi kua mshirika mzuri wa US, Osama bin laden aliwahi kua mshirika mzuri sana wa US kipindi cha mujahedeen nk. Wote walipomaliza kutimiwa walitupwa kama toilet paper.

Hivi unadhani mpaka lini Nato members watatumia kodi za wananchi kuifadhili Ukraine?
Zelensky upapet unamsumbua, ameicost nchi yake pakubwa sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom