nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,860
- 5,803
Mwandishi Wetu
Toleo la 289
10 Apr 2013
KWA mara ya kwanza katika historia ya kisiasa ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, kada wa chama hicho anatarajiwa kuteuliwa na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein, kuingia katika Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Raia Mwema, imebaini.
Gazeti hili limefanikiwa kupata nakala ya barua kutoka Ofisi ya Rais – Ikulu Zanzibar ya Machi 6, mwaka huu, kwenda kwa Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA ikitaka chama hicho kupendekeza majina mawili kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kabla ya Machi 13, mwaka huu ili uteuzi ufanyike kwa ridhaa ya Rais.
Taarifa zaidi zinaeleza ya kuwa kikao kilichofikia uamuzi wa kutaka kufanya uteuzi wa kada wa CHADEMA kilifanyika Machi mosi, mwaka huu kati ya Rais wa Zanzibar na viongozi wa vyama vya siasa. Kikao hicho kilihusisha mashauriano juu ya utekelezaji wa kifungu cha 119 (c) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
"Ilikubalika katika mkutano kwamba kila chama kiwasilishe majina ya watu wasiozidi wawili ili wawe miongoni mwa watu ambao Mhe. Rais anaweza kuwazingatia katika kuwateua wajumbe wawili wa Tume ya Uchaguzi kwa mujibu wa masharti ya kifungu 119 (c) cha Katiba ya Zanzibar ya 1984," inaeleza sehemu ya barua hiyo.
Barua hiyo yenye kichwa cha habari; kuwasilisha mapendekezo ya wajumbe wa Tume ya Uchaguzi kwa mujibu wa kifungu cha 119 (c) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, imetiwa saini na Dk. Abdulhamid Y. Mzee, ambaye ni Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi wa Zanzibar.
Mwandishi wetu alizungumza na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Hamad Yusuf, kuhusu suala hilo naye ingawa alikiri kuwahi kuwapo kwa kikao kati ya vyama vya siasa hiyo Machi mosi, lakini alisema suala la kufanya uteuzi ni la Rais wa Zanzibar, kwa hiyo hawezi kuzungumza chochote kuhusu hilo.
Tangu kuanza kuinuka kisiasa, CHADEMA haijapata mafanikio makubwa kwa upande wa Zanzibar ikilinganishwa na Tanzania Bara, licha ya kushiriki chaguzi mbalimbali za ubunge na ujumbe wa Baraza la Wawakilishi.