Rais wetu anashaurika, atazingatia haya njaa itaisha

Danfordkahwa

Senior Member
Mar 15, 2012
187
14
Tangu alipoingia madarakani Rais JPM Kutokana na mtindo wake wa kutumbua majipu baadhi ya watanzania walifurahia jinsi ya mfumo wa serikali ya awamu ya tano unavyoendeshwa kwa kutumbua bila ya kuzingatia sheria ya utumish wa umma.

Lakini sio dhumuni ya Makala hiii kueleza jinsi mfumo huo wa utumbuaji unavyoendeshwa bali ni kumshauri Rais wetu JPM kubadili sera yake ya uchumi hili sisi wanachi wa hali ya chini tupate kufaidika na hicho kinachosemwa na baadhi ya wachumi kuwa uchumi unapaa kwa asilimia 7.

Ni kweli uchumi unapaa kwa mujibu wa tafiti za Bank ya dunia na shirika la fedha la kimataifa IMF ambazo zinaonyesha uwekezaji ulivyokuwa kwenye sekta ya gesi na mafuta na madini. Lakini uchumi huu unaokuwa wanaonufaika ni vigogo wa serikali na wawekezaji kwsababu sheria ya uwekezaji aiwapi fursa wawekezaji wa ndani .hiii kutokana na baaada ya nchi nyingi za Afrika kuamua kuafata sera ya ubepari kati ya miaka 1980 na 1985 chini ya mashartiya IFM na bank ya dunia WB kuzinyonya nchi maskini.

Kipindi cha uongozi wa awamu ya nne wa Rais jakaya mrisho kikwete Bank ya Tanzania BOT ilikuwa ikiweka fedha zake kwenye bank za biashara ili bank fedha hizo ziweze kuwapatia mikopo wafanyabiashara wakubwa, kati na wadogo hili kuwepo na mzuzunguko mzuri wa fedha hapa nchini.Fedha hizo zilikuwa zinamfikia hadi mama ntilie kutokana mfumo mzima wa fedha.

Baada ya JPM kuingia madarakani alifuta mfumohuo wa bank kuu BOT kuweka fedha zake kwenye bank za biashara. Hali ya uchumi imekuwa mbaya wafanyabiashara wakubwa, kati na wadogo hadi mama ntilie hali imekuwa mbaya kutokana na mfumuko wa bei.

Nafahamu fika Rais wetu ni msikivu ndio maana alirudisha maadhimisho ya kumbukumbu ya kuzaliwa Tanganyika ambapo huadhimshwa kila ifikapo decemer 9 kila mwaka. Mwaka jana tulifanya usafi nchi nzima sikukuu aikufanyika lakini baada ya kupataushauri alirudisha kumbukumbu ya kuzaliwa Tanganyika.

Mfumo wetu ni private capitalism mfumo unamilikiwa na sekta binafsi serikali ubaki kuwa msimamizi na kukusanya mapato hvyo bila ya kujiwezesha bank za biashara kama ambavyo BOT ilivyokuwa inafanya kipindi cha Kiwete tumejilloga wenyewe.

Nchi yetu kamwe aiwezi kusonga mbele atupo kwenye mfumo wa kijamaa.
 
Mmmhhh! Ni sawa mkuu ataruhusu pesa zipelekwe kwenye hizo benki unazosema, lakini Mimi na wewe kwenye ile sehemu uliyosema juu ya utumbuaji majipu kidogo tunatofautiana, kivipi. Kabla ya JPM kuingia madarakani waliokua wanatumbuliwa ni wadogo wadogo tu hata Kwa kosa lakijinga wao watumbuaji bila kutambua nao itafika day, familia za wale wadogo wenye mishahara kiduchu walilia na wasijue pakuelekea tumewaona tena zaidi tofauti na hawa big fish ambao walishajiwekea mambo poa hata walivotumbuliwa familia zinaendelea kuneemeka tu kwani hizo sheria za utumishi Wa umma hazikuwepo!?
 
Back
Top Bottom