"Daraja la Mfugale pale, hujaliona? Wanafunzi wanasoma bure kabisa; Chekechea mpaka sekondari. viwanda tele kila kona. 'Nyerere hydroeletricity power' inajengwa, Madege kumi na moja yapo angani yetu, yamenunua kwa keshi, iiiii bagosha, acha nijimwambafai! Meli zimekamilika, barabara za 'interchange' kubwa Afrika pale Ubungo imekamika. Serikali kuu imehamia Dodoma. Bado watumishi hewa, mishahara hewa, wanafunzi hewa, laini hewa, mikopo hewa na hewa hewa zimetokomezwa kabisa chini ya utawala wangu, jamani bado tu, mjanielewa, niongezeeni miaka mingine mitano, muone maajabu, serikali ya Magufuli," alisikika mtumbuizaji moja anayetaka kufanana na Baraka Magufuli, akiwatambia wenzake.