Uchaguzi 2020 Rais wangu ukitaka tukuchague tena njoo na majibu ya kueleweka kuhusu haya maswali, bila hivyo hufai kuendelea

muafi

JF-Expert Member
Oct 6, 2015
2,074
4,693
Kama kweli unahitaji kuendelea kutetea kiti chako, Watanzania wanayohaki ya kufafanuliwa juu ya ahadi zako za mwaka 2015,

1. Mheshimiwa uliuahidi umma wa Watanzania kuwa katika utawala wako hakuna mfanyakazi ataedhulumika, utawalipa malupulupu yao, nyongeza ya mishahara, kupandishwa madaraja na kuongeza kima cha mshahara lakini mambo yamekuwa ndivyo sivyo.

2.Uliuahidi umma wa Watanzania kuwa katika utawala wako vijana watapata ajira na utawawezesha kujiajiri lakini mpaka sasa mambo yamekuwa ndivyo sivyo.

3. Uliuahidi umma wa Watanzania milioni hamsini kila kijiji kwaajiri ya vikindi vidogovidogo lakini mpaka sasa mambo yameenda ndivyo sivyo.

4. Uliuahidi umma wa Watanzania kuibadilisha Tanzania kuwa nchi ya viwanda lakini mpaka sasa umebaki ni wimbo tu, na baadhi ya viwanda vilivyofunguliwa ni vile vilivyo exist tangu zamani.

5. Uliuahidi umma wa Watanzania utaanzisha mahakama ya mafisadi lakini mpaka leo imekua ndivyo sivyo hata wale tuliokia tunaamini ni ni mafisadi papa bado wako uraiani wanakula bata, vile vile hata CAG alipozua ishu ya till1.5 kilichomtokea kila mtu anakijia

6. Uliuahidi umma wa Watanzania kuwa wanafunzi wa vyuo vikuu watapata mikopo asilimia zote na hakutakua na uzungushaji lakini matokeo yake kila mtu alishuhudia mpaka wenye vigezo walinyimwa kwa kisingizio wamesomea ahule za private.

7. Uliuahidi umma wa Watanzania utazingatia utawala bora kwa kifuata misingi ya katiba na sheria za nchi lakini kila mtu amejionea mambo yalivyokua ndivyo sivyo, kuna wakati katiba inakanyagwa kabisa hadharani na hakuna wa kuhoji.

Mheshimiwa wangu hayo ni machache tu miongoni mwa mengi, andaa majibu ya hayo utakapokuja kwenye kampeni utufafanulie kwanza jinsi ulivyotimiza hizo ahadi zako.
 
Ndugu ukielewa maana halisi ya poll tricks hutakuja kuhoji tena wewe sikilizia siku chama kikiwa na imani nae tena
 
Mheshimiwa wangu hayo ni machache tu miongoni mwa mengi, andaa majibu ya hayo utakapokuja kwenye kampeni utufafanulie kwanza jinsi ulivyotimiza hizo ahadi zako.
Maswali yako mepesi sana,naomba nimjibie mwenyekiti wangu
1.la mishahara na marupurupu limeshafanyika na linaendelea kwa waliobaki
2.Tumefungua milango na kutoa vitambulisho milioni moja ila mwenye nguvu ajiajiri kwa kupitia biashara ndogo
3.kuna mikopo ya wanawake na vijana kila halmshauri na marejesho wanafanya
4.mpaka tumeshafungua viwanda zaidi ya 2,000,data zipo Brela na TBS.
5.Tumeshika mafisadi yalioshindikana,tumebana majizi mpaka sasa yametapika Tsh bilioni 150
6.mikopo ni kwa wanafunzi waliosoma shule za serikali,haiwezekani babako kakulipia FEZA BOYS ada milioni 6,halafu unakuja kumenyana na watoto wa kipato cha chini
7.Nchi inaendeshwa kwa katiba na utawala bora ndio mana amani na utulivu,vimetamalaki
Ni vigumu sana kumfurahisha kila mtu ukiwa madarakani
 
No 1 hiyo,tumsamehe hakujua mkapa kama ataenda kupokonya ushindi Zanzibar..unaopelekea hadileo anahahaaaa fedha zamaendeleo,kibano alichopata kutoka nchi marafiki siomchezo...badala ziende tilion 11 kwenye maendeleo kulingana na bajeti pitishwa bungeni zinaenda tilion 3 ,unazani jambodogo mwaka huu zitaenda 2 ,mwaka huu magari yakubeba watu yatatoka wap

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Daraja la Mfugale pale, hujaliona? Wanafunzi wanasoma bure kabisa; Chekechea mpaka sekondari. viwanda tele kila kona. 'Nyerere hydroeletricity power' inajengwa, Madege kumi na moja yapo angani yetu, yamenunua kwa keshi, iiiii bagosha, acha nijimwambafai! Meli zimekamilika, barabara za 'interchange' kubwa Afrika pale Ubungo imekamika. Serikali kuu imehamia Dodoma. Bado watumishi hewa, mishahara hewa, wanafunzi hewa, laini hewa, mikopo hewa na hewa hewa zimetokomezwa kabisa chini ya utawala wangu, jamani bado tu, mjanielewa, niongezeeni miaka mingine mitano, muone maajabu, serikali ya Magufuli," alisikika mtumbuizaji moja anayetaka kufanana na Baraka Magufuli, akiwatambia wenzake.
 
kabombe,

Haya sio majawabu, bali ni majibu kwa mtindo wa propaganda. Ni hivi Magufuli sio rais mzuri wala bora, na hatakaa awe mzuri wala bora. Na kimsingi hana majibu ya maswali ya hivi na wala hayataki maana sio kiongozi anayejali utawala bora, bali anayeamini katika matumizi ya mabavu. Na hata hiyo 2020 hataweza kuheshimu box la kura, maana hana sifa ya kushinda kwa kura halali toka zamani.
 
Haya sio majawabu, bali ni majibu kwa mtindo wa propaganda. Ni hivi Magufuli sio rais mzuri wala bora, na hatakaa awe mzuri wala bora. Na kimsingi hana majibu ya maswali ya hivi na wala hayataki maana sio kiongozi anayejali utawala bora, bali anayeamini katika matumizi ya mabavu. Na hata hiyo 2020 hataweza kuheshimu box la kura, maana hana sifa ya kushinda kwa kura halali toka zamani.
Hayo ni mawazo yako endelea tu kuyadidimiza kwenye ubongo wak
 
Hayo ni mawazo yako endelea tu kuyadidimiza kwenye ubongo wak

Hayo niliyoyasema ndio ukweli wenyewe, japo ni ukweli unaokera. Hana uwezo wowote wa kushinda kihalali na ndio maana anategemea figusu zaidi kushindana, na hilo hajaanza baada ya kuwa mkulu, bali ni toka zamani. Kiongozi mwenye uwezo utamuona hata kwenye ujengaji wake wa hoja.
 
Mkuu ungesema wewe binafsi unatamani asirudi tena madarakani kwakua hajafanya hivi au vile, lakini huna uwezo wala uhalali wa kumpa Rais ultimatum yoyote

Na kwenye sanduku la kura kwa bahati(utachagua mwenyewe kama ni nzuri au mbaya) wanaochagua ni karibia milioni ishirini. Je? umeingia mawazoni mwao wote hao?!!!
 
Ulitegemea Rais aje hapa kukujibu?
Ungefunga comments ili tusichangie umsubiri tu huyo uliemuuliza
Umeambiwa Rais ajibu hayo anapoomba kura kwa wananchi, Mbona una kiherehere kama mkojo wew . Ivi huoni mtoa mada kaongea mambo muhim apo au ?
 
Ulitegemea Rais aje hapa kukujibu?
Ungefunga comments ili tusichangie umsubiri tu huyo uliemuuliza
Atakapokuja kwenye kampeni atueleze hizi ahadi zake amezitekelezaje sio anaonba kura tena ilihali ahadi za awali zimemshinda, pia hata wewe hapo sijaona ulichojibu zaidi ya upuuzi wa kujitoa ufahamu
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom