Mpendwa Rais heshima ulojipatia kwa jamii na Dunia nzima ya kutumbua majipu hakika imewafurahisha umma wote hasa watanzania wapenda mabadiliko. Lakini yote haya yameshanyewa na kutiliwa kinyesi na matendo ya wajinga au masalia ya mtangulizi wako JK ambae bila shaka 'kazi yako ya kutumbua majipu ' inamchukiza sana na hilo halina ubishi. Watanzania wengi wameshaanza kuwa na matumaini na wewe, ila imani hiyo kwa hakika imeanza kufifishwa na haya majipu mawili. Napenda nikujulishe kuwa hata asilimia 58% za kura ulizo pata kama ni kweli, basi ujue hiyo asilimia ndogo kiasi hicho ilitokana na watu hawa wawili. Chunga sana hawa ni ma-ajenti wa mafisadi na majipu makuu...chonde chonde baba amka na fanya jambo upesi ...au unasubiri mpaka uwe mwenyekiti wa chama hicho cha majipu- CCM? Ni hayo tu kama nimekuudhi niisamehe huu ni mtazamo wangu na kautafiti nilikofanya ka harakaharaka! Matendo mabaya yaliyofanywa na Nape ni kama - Uswahili uliyofanya CCM kuonekana chama kisichokuwa na thinkers, Kufungia vyomba vya habari na hii kusema TBC isioneshe mwenendo wa Bunge mojakwamoja yaani Live! Kwa upande wa Chenge - Wizi wa mali za umma - nukuu 'ESCROW scandal', Ishuu iliyo mpelekea akabatizwa mzee wa 'vijisent' n.k. Hawa wawili hawana intergrit katika umma wa Dunia na watanzania...!!