General Mangi
JF-Expert Member
- Dec 21, 2013
- 15,303
- 23,058
Rais wangu Dr. John Magufuli kwanza nakupongeza kwa dhati kuzungumza kweli bila kupepesa.
Jana uoongea kauli nzito ambayo ni mataifa masikini Ma Rais wao huogopa kuieleza kwa wananchi.
Uligusia jinsi nchi kama Sudan Kusini kupata uhuru wao lakini kutokana na kuwepo kwa mafuta basi Nchi kubwa za nje zimekuwa zikileta mgogoro wa wenyewe kwa wenyewe kugombana. Uligusia mifano kadhaa na hata kutoa tahadhari kwa sisi watanzania tuwe makini.
Ni kweli kwamba migogoro mingi inayoendelea Syria, South Sudan, Libya, Yemen ni kutokana na Mafuta waliyo nayo.
Ni vizuri umeliweka jambo hili bayana ili kila mtanzania awe makini nalo kuepuka chokochoko ambazo zinaweza kuteta mgogoro baina yetu.
Ni wazi kwamba haya yote Wapinzani wanatamani yatokee kwa ulafi wa kukaa hapo Magogoni.
Sisi tukiwa watanzania tunao taka amani tunaomba uzidi kuhakikisha mataifa hayo hayapati fursa kama hii hapa nchini.
Mungu akulinde na akujaze Nguvu kuiletea maendeleo nchi yetu.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.