Rais wangu JK: Watanzania wanakufa Ujerumani, tafadhali chukua hatua ya haraka kuwaokoa

Nilipata hiyo post kusoma PHD kwa DAAD nikashauriwa niiturn down. Kumbe sikukosea. Nasoma uzamivu hapa hapa bongo. Ulaya ya sasa naijua si ya kukimbilia. Poleni wahusika.
 
Kucheleweshwa mwezi mmoja kulipwa stahiki zao kwa huko ugenini ni tatizo, lakini mimi mtazamo wangu sioni kama ni tatizo lililoshindwa kutatulika hapa chini hadi kuamua kumfikia rais,

Kile unachokiita ni juhudi za kufuatilia mimi naona sio juhudi stahiki mkuu,

Kwanza huku ughaibuni kituo cha kwanza na mujarabu kabisa ni ubalozi wa nchi yenu huko mliko,

Tueleze kwanza Balozi wa Tanzania bwana Philipo Marmo amewaambia nini juu ya suala lenu mpaka mkaamua kulipeleka kwa rais?

Mnatambua wenzenu huku nyumbani pesa zao (mabumu) zinachelewa kwa miezi 3?

Mnatambua kuwa wazazi wenu mishahara ya serikali inachelewa bila sababu za msingi?

Suali hilo sio lenu tu ni suala la nchi nzima, taifa limekosa uwajibikaji kwa kila mtu kuanzia mjumbe wa nyumba kumi hadi rais wa nchi!

Pole yao, nawashauri nendeni Ubalozini mkamuone Marmo uso kwa uso na mmwambie wazi kuwa akishindwa kuwashughulikia mgawane mshahara wake!
 
Sitaki kusema mengi kwa sababu maalum.

Tatizo halipo TCU tatizo lipo MOEVT.
Suluhisho ni kutopitishia hiyo fund MOEVT iwe TCU moja kwa moja.
Mwenye sikio na asikie!
 
Tunamtaka Membe hapa jamvini atupe msimamo wa serikali,hii ni aibu ambayo haivumiliki Lazima wanafunzi wapate hela kwa wakati,pale hazina watu wamelala tu hawafanyi kazi
 
Poleni sana wanafunzi Rais wetu ni msikivu na imani suala hili limeishamfikia na atalitatua.

Haha...unavyoongea km wewe una hakika rais kasikia....

Kwa wana saikologia si ngumu kumuona kichaa.....vichaa wa aina yako vitu vyote vilivyopo upande wao husema vinawezakana,vitafanyika na ahadi kibao..ila ktk ufuatiliaji na kuwajibika yasipofanyika.Hukaa kimya bil amipango yoyote ila bado wataendelea kusema subiri yatafanyika.

Insanity ni tatizo la CCM na raia walioambukizwa....siku zote hudhani mambo yatafanyiak yenyewe hata wasipofanya kitu kipya wala chochote.

wewe unadhani huo usikivu wa rais umekuja lini na nini katatua....last time nakumbuka nilisikia bungeni "Serikali Sikivu" lilitamkwa kama mzaha na wabunge wa CCM haswa yule wa kule rukwa.
 
Mzee,
Nimejaribu kuongea na broo kuhusu hilo la kutafuta kazi, naye kasema kwamba kazi kwasasa Ujerumani si rahisi kupata hata ya usafi kwani Waturuki na watu toka nchi za ulaya mashariki (kama Poland, Slovenia, Slovakia, n.k) wamejazana sana Ujerumani kufanya hizo kazi.

Ndugu yango ulichoandika ni kama unazidi thibitisha kuwa watanzania ni useless..hawa jamaa ni wasomi pengine cream ya nchi..Halafu hawawezi fanya kitu tofauti na routines ambazo mtu asiyejitambua u kuw ana malengo anaweza fanya.

Yaani huyo bro wako hajaweza evaluate mazingira yake na uweo binafsi, majukumu yake kwa taifa na kujua wapi anahitaji kuonyesha competitiveness yake?

Hata ndnai ya TZ watanzania wanalia dhidi ya wakenya, wapakistan, bangladesh, waganda, warundi na wengine wanaingia nchini kwa fujo....Ni jukumu lao kubadili fikra za wajerumani ili wavutiwe kuwaaajiri watanzania....

MWAMBIE KAKA YAKE LAZIMA A SURVIVE HATA KM SERIKALI YA JK IMEZIMIKA AU HATA WENGINE WANACHUKUA KAZI UJERUMANI.Otherwise hafai, anafanya tafiti za nini?na anasoma ili afanye nini km hawezi jikomboa mwenyewe atamkomboa nani?
 
Pole yao, nawashauri nendeni Ubalozini mkamuone Marmo uso kwa uso na mmwambie wazi kuwa akishindwa kuwashughulikia mgawane mshahara wake!
Mshahara wake hata auitajiki awagaie tu mpunga wa VISA za watalii, jamaa wanakusanya hela mingi sana. Sijui kwanini wanataka vijana wateseke kwenye ardhi za watu.
 
Hiii taabu kweli kila kitu kutupiwa rais, Kwani huko Ujeremani hatuna Ubarozi,

Pia hawa watu ni watumishi wa vyuo tena taasisi zinazolipa vizuri watumishi wake wanawajaili wakiwa kwenye lecture theater tuu wakiwa nje ya majukumu ya kawaida hawawasaidii kwa lolote.

Wameongea na waajiri wao pengine wangepata msaada.
Mkuu nadhani imeelezwa vizuri sana mada tena kwa kina . Inaonyesha hapa wa kulaumiwa ni MOEVT/TCU ambao hawakutimiza wajibu wao. Sasa hapo tatizo sio mwajili.
 
Poleni sana wanafunzi Rais wetu ni msikivu na imani suala hili limeishamfikia na atalitatua.

Ni msikivu na msemaji ila sio mtekelezaji hata chembe.. Nawapa pole wahanga.
 
Ndugu yango ulichoandika ni kama unazidi thibitisha kuwa watanzania ni useless..hawa jamaa ni wasomi pengine cream ya nchi..Halafu hawawezi fanya kitu tofauti na routines ambazo mtu asiyejitambua u kuw ana malengo anaweza fanya.

Yaani huyo bro wako hajaweza evaluate mazingira yake na uweo binafsi, majukumu yake kwa taifa na kujua wapi anahitaji kuonyesha competitiveness yake?

Hata ndnai ya TZ watanzania wanalia dhidi ya wakenya, wapakistan, bangladesh, waganda, warundi na wengine wanaingia nchini kwa fujo....Ni jukumu lao kubadili fikra za wajerumani ili wavutiwe kuwaaajiri watanzania....

MWAMBIE KAKA YAKE LAZIMA A SURVIVE HATA KM SERIKALI YA JK IMEZIMIKA AU HATA WENGINE WANACHUKUA KAZI UJERUMANI.Otherwise hafai, anafanya tafiti za nini?na anasoma ili afanye nini km hawezi jikomboa mwenyewe atamkomboa nani?
Mkuu umeeleza vizuri lkn unasahau kua nchi za wenzetu wanathamini sana watu wa kwao na ili upate kazi yoyote lazima uwe na network hawaamini watu kirahisi. Kwa mtazamo wangu kama waliaidiwa kulipiwa hiyo 80% muhusika ni vema akalipa sababu kiwango hicho ni kikubwa sana. Na kama watajikita ktk kufanya survival jobs watajikuta wanashindwa kupata walichofuata. Upatikanaji wa kazi si rahisi kama tunavyofikiri na gharama za maisha ziko juu sana kuliko hapa bongo.
 
Ila hawa jamaa nyanya sana, yani pamoja na kupewa 80% na wajerumani na Mishahara naamini inaendelea kuingia kama kawaida kwani ni watumishi wa serekali hawa. Lakini bado wanalialia.

Wakati kunawatu huku hawajapata hata hiyo 0% toka TCU na wanakomaa na kitabu mwendo wa pasi ndefu na kudownload maji.

@∆ibanga Ampiga Mkoloni, mbona unasoma bila kuelewa? Ni kwamba tunalipwa na Ujerumani 20%, hiyo 80% ndiyo inatoka serikalini. Halafu hiyo pesa yenyewe huwezi kusave, maana pango, semester fees that including semester ticket, na gharama nyingine ni kwetu.
 
Siku nyingine mkipata nafasi za kwenda nje pitieni kwenye vijiwe vya watoto wa mujini mjifunze mbinu nyingine za kuishi nje za nchi.

...kati ya hao wanafunzi kuna ambao wanasoma mwaka wa tatu sasa, miaka mitatu Ujerumani bila ya kuwa na connection ya japo kijikazi cha kuosha vyombo kwenye migahawa ya Kebab si rahisi kumtokea mtoto aliyetokea "kijiweni" hata kukiwa na Wapolish,Wabulgaria,n.k wa kumwaga (Waturuki wapo wengi Ujerumani tokea zamani sana)!

Pia kuna tatizo kwa Watanzania wengi (si wote) ku-intergrate katika nchi wanazoishi.

Vinginevyo natumai kuwa matakwa yenu (waathirika)yaliyo katika mikataba yatatimizwa haraka!

Nafikiri wengi wenu mnachangia kutafuta vibarua Ujerumani mkiwa na Experience ya US ama UK. Huku ni ngumu sana kupiga BOX. Pia shule ipo tight sana. Kwanza PhD za huku zina Course work na weengi wetu tuna kazi za maabara, then ufanye analysis, uattend course work, usome na kuandika papers, uattend semina nk. Kwakweli huo muda hautoshi, na tukisema tupige BOX tutakaa zaidi ya mikaa minne. Hivyo tunafanya kazi usiku na mchana ili tumalize hii shule mapema na kuondokana na haya mateso.
 
Mkuu umeeleza vizuri lkn unasahau kua nchi za wenzetu wanathamini sana watu wa kwao na ili upate kazi yoyote lazima uwe na network hawaamini watu kirahisi. Kwa mtazamo wangu kama waliaidiwa kulipiwa hiyo 80% muhusika ni vema akalipa sababu kiwango hicho ni kikubwa sana. Na kama watajikita ktk kufanya survival jobs watajikuta wanashindwa kupata walichofuata. Upatikanaji wa kazi si rahisi kama tunavyofikiri na gharama za maisha ziko juu sana kuliko hapa bongo.

Nimeelewa sana.....ndio maana nimeongelea issue ya competition ktk kazi.Hao jamaa huko walipo walichobaki nacho ni ama kukaa bure, ama kuingiza chochote cha kuwasaidia km akiba, au hata kusoma ikiwezekana ama pia kusecure deal ya kazi km issue itaishia kuwa warudi nyumbani.Au serikali ikope kwa wajerumani.
 
Unajua huu utaratibu wa kufanya mambo bila mipango endelevu ni taabu sana . Sasa kama wahusika waliona watashindwa tangu mwanzo basi ni bora wasingewapa hizo nafasi manake waliowaacha huku nyuma wamepiga hatua japo kidogo kufulia ugenini ni noumaa mkuu. Asane mkuu lkn inaumiza sana nawapa pole hao watz .
 
CCM ni mambo yao ni km mimba iliyotunga ktk mirija vibaya..wanafanya kitu wakiwa wameshakiharibu kwanza.ENDELEVU NI KITU iliyoingia kimakosa ktk dictionary ya kiswahili...pengine si tafsiri ya sustainable ...ndio maana huwa linaeleweka tofauti.
 
Nafikiri wengi wenu mnachangia kutafuta vibarua Ujerumani mkiwa na Experience ya US ama UK. Huku ni ngumu sana kupiga BOX. Pia shule ipo tight sana. Kwanza PhD za huku zina Course work na weengi wetu tuna kazi za maabara, then ufanye analysis, uattend course work, usome na kuandika papers, uattend semina nk. Kwakweli huo muda hautoshi, na tukisema tupige BOX tutakaa zaidi ya mikaa minne. Hivyo tunafanya kazi usiku na mchana ili tumalize hii shule mapema na kuondokana na haya mateso.
PhD zote ni ngumu, lakini lazima muwe wabunifu kutokana na hali halisi. Mnao muda wa kutosha kuchacharika na kujipatia kipato. Acheni kulalamika tafuteni solution, ndio maana ya Ph D
 
Back
Top Bottom