My Son drink water
JF-Expert Member
- Nov 30, 2016
- 4,930
- 13,335
Rais wangu Magufuli, kwanza kabisa Nakutakia heri ya mwaka mpya pamoja na familia yako yote.
Najua wazi kuwa una nia njema Sana na taifa letu Tanzania .
Rais wangu, Nakuomba Sana utenganishe mamlaka ya serikali na mamlaka ya Mungu.
Kanisa ni kanisa, na serikali ni serikali, hivi vitu viwili kamwe havioani ni maji na mafuta kabisa.
Japokuwa serikali ndo inachapisha pesa na kuzidhibiti lakini neno la Mungu linasema kwamba.
"Fedha ni mali yangu, na dhahabu ni mali yangu, asema BWANA wa majeshi "Hagai 2:80.
Rais wangu, kauli yako uliyoitoa kanisani Bukoba kuwa watumishi wa MUNGU wakuvumilie Kwa Sababu hata makanisani pesa zitakauka, haikuwa kauli nzuri kutolewa na mcha Mungu Kama wewe.
Rais wangu, pesa zitakauka pote, lakini hazitakauka makanisani wala misikitini, ni Kwa Sababu hayo ni mahekalu ya Mungu ambaye pesa ni mali yake.
Rais wangu, makanisa na misikiti yahahitaji pesa ili kazi ya Mungu iweze kufanyika, watumishi Wa Mungu hawahusiki na ufisadi uliokuwa ukifanyika, wao wanataka pesa ili Waitangaze injili ya Mungu wetu aliye juu mbinguni.
Na Mungu hawezi kukubali watumishi wake wakose pesa za kuhubiri neno lake.
Ni Kwa Sababu pesa ni mali yake.
Rais wangu, ni kweli kabisa nchi ilitapakaa wapiga dili, lakini walikuwa wangapi ktk raia wote mil 38 wenye akili timamu?
Rais wangu, napata shida Sana kuamini kuwa kila mwananchi anayelia shida alikuwa mpiga dili.
Rais wangu, nililima vitunguu vikaozea shambani Kwa Sababu ulizuia mazao yasiuzwe nje ya nchi.
Nikawa nimepata hasara ya mil 30,hali hiyo ilinifanya kuyumba na kuanguka kabisa kiuchumi, Kwa mantiki hiyo Rais wangu na mimi nilikuwa mpiga dili?
Rais wangu, mbiu ya mnyonge ipigwe sasa, Kwa Sababu Naamini bado kuwa wewe ni rais wa wanyonge, watu watoke kaskazini, Kusini, mashariki na magharibi na kisha kila mmoja amtaje mpiga dili, na hao wapiga dili wakamatwe na kushtakiwa na kisha siye tunaoishi Kwa jasho letu tupumue sasa.
Maana tumechoka kusikia kuwa wanaoteseka na hawaioni pesa ni wapiga dili.
Rais wangu, kuna wakati wa Mungu na wakati wa mwanadamu.
Tulionao ni wakati wa mwanadamu, ndo maana tunaambiwa hata wale wafanyabiashara 320 waliofunga maduka yao Kwa Sababu ya kushindwa kuendelea na biashara Kutokana na kupanda Kwa kodi eti nao ni wapiga dili.
Rais wangu, wako wapi hao wapiga dili ili waende jela siye tupumue?
Rais wangu, usikubali watu wabaya wakauleta wakati wa MUNGU ktk Uongozi wako, MUNGU huyu anatisha Sana, anaogofya Sana, njia zake, matendo yake kamwe hayachunguziki hata kidogo.
Rais wangu, Kwa Sababu wewe ndo mkuu wa nchi lolote linalotokea hata Kama hujahusika utawasikia wakisema ni Magufuli tu.
Rais wangu, jina lako limo midomoni mwa watanzania Kwa mema na mabaya.
Rais wangu, simama sasa ili tupate ahueni ya maisha.
Makanisa na misikiti yaache, hayo hayawezi kukaukiwa pesa Kwa Sababu hayana uhusiano na mambo ya Kidunia, yapo Kwa ajili ya kazi ya Mungu tu, na Mungu mwenyewe ndo anayasimamia.