TIGOPESA
Senior Member
- Apr 2, 2014
- 190
- 64
Mwanasheria mkuu wa Zanzibar anasema hati ziko UN
Katibu wa bunge maalumu anasema hati ipo mahkama kuu Dar
Ina maan kila mmoja anasema bila ya kuwa na uhakika. Kila kinachokuja mdomoni tu ni kusema tu bila kuangalia athari zake kwa umma. Hawana kisisi wala gatigati kwa yanayowatoka midomoni bila ushahidi kama ni kweli au uongo kwa sababu wanaona hakuna wa kuwawajibisha. Serikali na Muungano ni wa CCM kwa hivyo wao kukosa maadili si kitu kikubwa ni mambo ya kawaida tu.
Na hapa ndiyo naunganisha na yale yanayotokea katika majukwaa ya kisiasa Zanzibar ya akina Shaka, Sadifa, Borafya, Shamte na wengine wengi kutukana mbele ya halaiki ya watu matusi ya nguoni. Mtu mwenye maadili hawezi kutukana mbele za hata mtoto mdogo. Hii inaoneshea ni moja ya falsafa ya CCM. Kukosa maadili kwao siyo tatizo hata kidogo. Inaoneshea kukosa maadili ni "credit" kwa CCM na hasa unafaa kwa uongozi wa juu.
Hapa vile vile ndiyo ukaona hata hao wafanyakazi wa mahkama kuu au AG hawakuona jambo kubwa kughushi sahihi za hati ya muungano. Jamani hii ni "crisis" kubwa ya taifa, jamii na mfumo wote wa mahkama na sheria za Tanzania. Kama leo nyaraka muhimu kama hizi na kutoka ofisi ya AG zimeghushiwa sahihi je mambo yanayowahusu wananchi wa kawaida.
Na bahati mbaya Sammuel Sitta anaona ni very simple jambo hili halichukulii katika uzito wowote kuwa un "tarnish negatively" mfumo mzima wa serikali. Lakini hapa linaturejesha tena palepale CCM hawana maadili na wametujengea mfumo ambao watu hawajali maadili.
Naam ni kama Waswahili wanavyosema "Ukiona kilemba kimeroa basi ubinda (underwear) hautazamiki" Sasa ikiwa watu wa juu wa CCM wako hivi je hao wa chini watakuwaje? Na CCM wasikwambie watajirekebisha, hawawezi kujirekebisha mpaka kwanza wawe nje ya uongozi hawa.