Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,778
- 218,404
Hii ndio Taarifa mpya ya leo kutoka mjini Bukoba , kama ilivyosambazwa na Mwananchi Digital .
Zaidi jionee Mwenyewe
Kigogo wa zamani wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Gratian Mkoba amejitokeza kuchukua fomu kuwania uenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), mkoa wa Kagera.
Mkoba, aliyewahi pia kuwa Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta), amechukua fomu hiyo, Machi 13, 2024 katika ofisi za Chadema mkoa wa Kagera zilizopo manispaa ya Bukoba.
Akizungumza na Mwananchi Digital leo Ijumaa, Machi 15, 2024, Mkoba amesema licha kuhudumu nafasi mbalimbali, lakini alikuwa katika siasa, akisema siasa ni maisha huwezi kuiacha hadi mtu akifariki dunia.
Amesema kuanzia asubuhi, kuamka, kushinda, kutembea, kula na kulala ni siasa na unapofanya kazi pia ni siasa.