G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,555
- 35,880
Rais wa Uswis ndugu Alain Berset amekaa nchini Tanzania kwa takribani wiki mbili na kuondoka bila kuonana na Rais mwenzake ndugu John Pombe Magufuli. Alipokewa KIA na waziri mkuu na kuagwa na waziri wa mambo ya nchi za nje.
Lipo tatizo?
Ndiyo, haiwezekani miongoni mkubwa wa nchi kama Uswis anakuja na kuondoka kimya kimya ndani ya nchi kama Tanzania bila kubadilishana walau mawazo mawili ma tatu na rais mwenzake ili kutengeneza fursa mbalimbali. Kuna tofauti kubwa kati ya rais na mawaziri na ndiyo maana tukasema "Nchi iwe na rais kama kiongozi mkuu" Huyu popote pale atakapoongea ujumbe wake utakuwa tofauti sana na walio chini yake.
Hii tabia ya Rais Magufuli kukwepa kwepa viongozi mbalimbali wenye ushawishi duniani inatupelekea ujumbe kuwa pengine hatuna mtu wa aina ya wenzake huko duniani katika kiti hicho. Anakuja rais wa Uswis tunakwepa kwepa kuonana naye kisha anakuja rais wa Ethiopia huyo tunamuomba hadi mikopo. Zaidi amekuja kwenye huo utalii hata waizir mwenyewe mwenye dhamana ya huo utalii hakutaka kubadilishana naye mawazo na kupata fursa zaidi. Yupo huko anajiita "Mzee wa pori kwa pori" Anafanya ziara ambazo kama waziri hazina maana wala ufanisi wowote ule kwenye kuendeleza sekta hii muhimu nchini.
Mbaya zaidi ni nadra sana kwa huyu kiongozi kutembelea nchi yetu kikazi. Moja ya neno "mchapa kazi" ni kuitumia fursa mahali ambapo ni vigumu kuitumia! Tunaita kupaa kwa kutumia mikono! Huyu kiongozi hata kama kaja kwa mambo binafsi, ingetosha tu kumualika ikulu au hata Pombe John Magufuli angetumia usafiri wa helkopta kumfuata huko mbugani ili atumie nafasi vizuri! Huyo ndiye kiongozi anayeitwa mchapa kazi! Siyo hizi tunazoona.
Hata kama ni mimi amekuja Bilgate kwenye pori langu kuangalia nyasi basi nitakuwa mjinga sana kuwaacha tu wanangu wampokee na kumalizana naye eti kwakuwa hakuja kwa ajili yangu! Nitakuwa sijaitendea haki fursa ya uwepo wa lile pori. Rais awe popote pale duniani atabaki kuwa Rais. Kwa viongozi wa nchi kama Uswis kutokutumia fursa hadhimu kama hizi kuwaona popote pale walipo kwa urahisi wa aina hii kwa visingizio visivyo na mashiko hakutuondolei kuitwa "Wazubaifu tuliopitiliza"
Tusijidanganye! Bado sisi ni nchi changa tena sana! Tuachane na zile tambo za kanda ya ziwa.

Last edited: