Rais wa Ufaransa ziarani Saudi Arabia....

Rais wa Ufaransa ziarani Saudi Arabia....

Jambazi

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2014
Posts
16,654
Reaction score
18,805
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron
_98691462_31c82443-4425-445d-b3e2-35667b832658.jpg

ambaye yuko nchini Saudi Arabia katika ziara isiyopanga, amesema atasisitizia umuhimu wa utulivu nchini Lebanon, katika mazungumzo yake na na viongozi wa nchi hiyo.

Ufaransa ina uhusiano wa karibu na Lebanon, na ziara hiyo ya Rais Macron imekuja siku moja baada Waziri mkuu Saad Hariri, kujiuzulu wakati alipokuwa Riyadh, hali inayochochea hisia kwamba alishinikizwa na Saud Arabia. Awali akizungumza mjini Dubai, Rais Macron amesema anataka viongozi wa Lebanon kuishi huru ndani ya nchi yao.

Amesema pia atautaka uongozi wa Saud Arabia kusaidia kuzuia baa la njaa nchini Yemen, ambako muungano wa majeshi yanayoongozwa na nchi hiyo yamefunga bandari kuzia silaha kuingizwa nchini humo na kuwafikia wapiganaji wa Ki Houthi.
 
Back
Top Bottom