WILSON MWIJAGE
JF-Expert Member
- May 30, 2011
- 276
- 78
Abdoulaye Wade (85) ambaye ni Rais wa Senegal anavunja katiba, Rais huyo alipoingia madarakani aliifanyia mabadiliko katiba ya nchi yake na kuweka utaratibu kwamba Rais atakaiongoza Senegal ataiongoza kwa kipindi cha awamu mbili tu. Vipindi viwili kwa Rais huyo vimeisha kuiongoza Senegal, lakini analazimisha kuwania tena urais wa nchi hiyo kwa awamu nyingine hati tu kwasababu sheria hiyo haikuwepo wakati anaingia madarakani. Je hii ni huruka ya binadamu au ni huruka ya viongozi wa ki-Afrika ya kutoheshimu sheria, taratibu na kanuni za nchi zao au ni ualafi wa kutojali matakwa ya wananchi? Taarifa zilizopo ni kwamba kwa sasa wananchi wa Senegal wamezusha taflani na fujo kubwa wakipinga hali hiyo.