Rais wa Rwanda, Paul Kagame kufungua maonesho ya Sabasaba. Kufanya mazungumzo na Rais Magufuli

Chabruma

JF-Expert Member
Sep 19, 2013
5,660
1,780
RAIS KAGAME KUFUNGUA MAOENESHO YA SABASABA.





Rais Kagame kufungua Maonesho ya 40 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba).
Mhe. Paul Kagame, Rais wa Jamhuri ya Rwanda anatarajiwa kufanya ziara rasmi nchini tarehe 01 Julai 2016 kufuatia mwaliko kutoka kwa Mhe. Dkt, John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akiwa nchini Mheshimiwa Rais Kagame atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake, Mheshimiwa Rais John Pombe Joseph Magufuli na baadaye kwa pamoja viongozi hao watashuhudia uwekaji saini wa Makubaliano ya Pamoja (MoUs) baina ya Tanzania na Rwanda katika sekta mbalimbali za ushirikiano.

Aidha, Mheshimiwa Kagame atashiriki dhifa rasmi ya kitaifa itakayoandaliwa kwa heshima yake na mwenyeji wake Mheshimiwa Rais Magufuli .
Mchana wa tarehe 1 Julai, 2016 Mheshimiwa Rais Kagame akiambatana na mwenyeji wake atahudhuria maonesho ya 40 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) kama Mgeni Rasmi kwa ajili ya kuyafungu.

Ziara hiyo ya Mheshimiwa Kagame inafuatia ziara yenye mafanikio aliyofanya Mhe. Dkt. John Pombe Jospeh Magufuli nchini Rwanda mwezi Aprili 2016. Ziara hiyo ni ishara nyingine ya kuimarika kwa mahusiano baina ya nchi hizi mbili.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Dar es Salaam, 23 Juni 2016.
 
Lipumba naye wakati wa uchaguzi alienda Rwanda......siku chache baada ya kagame kumtishia JK tumependana balaa....tena ghafla
 
Rwanda na Tanzania Ziungane iwe nchi moja.
Rwanda sasa hivi imetulia wana amani kama walivyo wa Tanzania.Hawajazalisha wakimbizi kwa kipindi kirefu.Napendekeza bunge la Rwanda lianze mchakato wa kuunganisha Tanzania na Rwanda tuwe na nchi moja (superpower afrika mashariki na kati)

Hebu fikiria Raisi wa hiyo nchi awe magufuli makamu awe kagame au raisi awe kagame makamu wake Magufuli nani atatukuta kimaendeleo? Tutapaa mbio kimaendeleo
 
Rwanda na Wanyarwanda ni mfano mzuri wa namna watu wanavyoweza kubadilika na kubadilisha maeneo yao kutoka bonde la mauti hadi kuwa 'nchi ya ahadi'. Kuna jambo la kujifunza kutoka kwa Kagame na wanyarwanda kwa ujumla.
 
Tuipige , na nani we mpinga juhudi za rais au hivi kweli we we unataka maendeleo ya haraka kweli kila kit kupinga ndio maana rais amesema msimcheleweshe name uchaguzi umekwisha salsa no kazi tu
 
Rwanda na Tanzania Ziungane iwe nchi moja.
Rwanda sasa hivi imetulia wana amani kama walivyo wa Tanzania.Hawajazalisha wakimbizi kwa kipindi kirefu.Napendekeza bunge la Rwanda lianze mchakato wa kuunganisha Tanzania na Rwanda tuwe na nchi moja (superpower afrika mashariki na kati)

Hebu fikiria Raisi wa hiyo nchi awe magufuli makamu awe kagame au raisi awe kagame makamu wake Magufuli nani atatukuta kimaendeleo? Tutapaa mbio kimaendeleo
Hatutaki
 
Back
Top Bottom