Rais wa DARUSO amtumbua Martine Malisa kwa ufisadi

Rais wa DARUSO amtumbua Martine Malisa kwa ufisadi

KADA08

Member
Joined
Dec 2, 2017
Posts
44
Reaction score
153
Taarifa iliyotolewa na katibu mkuu ofisi ya rais DARUSO inasema rais wa serikali hiyo ya wanafunzi Ndg Jeremiah Jilili ametengua uteuzi wa Ndg Martine Malisa B, kama mbunge wa kuteuliwa na rais, waziri wa habari, mawasiliano, mambo ya nje na jumuiya za wanafunzi kuanzia leo kwa kutafuna fedha taslimu milioni moja alizopewa tangu tarehe 22/12/2017 kutokana na bajeti kwa ajili ya kutengeneza mbao za matangazo na website ya DARUSO.

Pamoja na kutenguliwa Ndugu Malissa ametakiwa kurejesha kiwango hicho cha fedha haraka iwezekanavyo kwani ikishindikana atapoteza masomo yake na kushtakiwa kwa uwizi wa fedha za umma.

Rais wa DARUSO ambaye amejipambanua kama kada wa CCM amepongezwa kwa msimamo wake katika kusimamia maslahi ya wanafunzi, kupiga vita ubadhirifu, ufisadi na usimamizi dhabiti wa maadili na uzalendo katika serikali yake.

Inaelezwa Ndugu Jilili ni moja ya watu wanaovutiwa sana na utendaji wa Rais Magufuli hivyo anamuishi kwa vitendo kama role model wake.

Solidarity.... Forever
IMG-20180417-WA0219.jpg
 
Daruso kuna Rais? Daruso ilishaisha siku nyingi hakuna vichwa hapo siku hizi nyie madogo wote hakuna kitu mnambwela mbwela tu hamuwezi kusema kitu cha maana kusaidia nchi zamani hapo Rais ni maarufu nchi nzima hii Rais wa Daruso anajulikana.saiv mnacheza makida tu
 
Maisha Yanabadirika Mkuu
 
Back
Top Bottom