#COVID19 Rais wa Chama cha Madaktari (MAT): Muitikio wa kupata chanjo hauridhishi, elimu itolewe

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
Akizungumza na Mwananchi jana, Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk Shadrack Mwaibambe alisema idadi hiyo ni ndogo ukilinganisha na idadi ya watu katika makundi yaliyolengwa.

“Tulivyopokea dozi 1,058,400 nilitarajia hizo zisingetosha, lakini cha ajabu mwitikio umekuwa mdogo, Serikali inapaswa kutambua kwamba kinachotakiwa kufanyika sasa ni kuwekeza kwenye elimu,” alisema.

Dk Mwaibambe alisema kuna kundi kubwa la Watanzania ambalo lipo katikati halijajua bado kama litachanja au halitachanja hilo linahitaji kufikishiwa elimu.

“Kuna kundi dogo ambalo lilihitaji chanjo na limechangamkia fursa na kundi jingine dogo la wanaopinga na hao wanaendesha kampeni kupitia simu janja na kampeni hiyo inawaathiri wale ambao hawajajua watafanya nini, wanasita kwenda kupata chanjo na ndani ya hilo kundi pia wapo ambao hawajapata elimu na wengine hawajui wapi wakapate chanjo,” alisema.

Alisema makundi ya Watanzania wote yaangaliwe bila kujali wanaishi mijini au vijijini ili kila mmoja atumie haki yake kupata chanjo, “Serikali iandae mkakati mkubwa kuwafikia ukiangalia vituo vilivyotengwa ni 550 pekee na tunavyo vituo zaidi ya 7000 vya afya kote nchini na hapo kuna vijiji havina zahanati utaona kuna kundi kubwa halijui zitawafikiaje, lakini Serikali inazidi kuongeza vituo.”

Dk Mwaibambe alitaja sababu nyingine kuwa ni chanjo kufikishwa mapema kabla wananchi hawajapata elimu ya kutosha.

“Tuliambiwa ingefika Oktoba lakini bahati nzuri imekuja mapema wakati bado hatujawekeza katika elimu, kwani hatujafikia makundi mengine ambayo hayana muda wa kusikiliza redio wala kuangalia TV na elimu inatolewa asubuhi wakati watu wapo makazini na kwenye vibarua, tuwekeze katika utoaji elimu,” alisema Dk Mwaibambe.

Taarifa ya Wizara
Taarifa iliyotolewa jana na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Profesa Abel Makubi kuhusu maendeleo ya utoaj wa chanjo ya Uviko-19 kwa wananchi ilieleza kuwa Serikali inaendelea kuratibu utoaji wa chanjo hiyo kwa hiari kupitia vituo vya kutolea huduma za afya vya umma na binafsi 550 vilivyoidhinishwa hapa nchini.

Profesa Makubi alizitaka mamlaka za mikoa, wilaya na mitaa kwa kuhamasisha zoezi la chanjo na pawepo pia na juhudi zaidi za kuongeza kasi katika maeneo ya pembezoni ya miji, mitaa na vijijni na kuwataka wataalamu wa afya kuelimisha jamii.

Umuhimu wa chanjo
Sheria ya afya ya umma, namba 1 ya mwaka 2009, inaelekeza kuwa chanjo ni lazima kwa ugonjwa wowote ambao umeonekana kuwa tishio na ambao imethibitika kwamba chanjo ni njia mojawapo ya kupunguza kasi ya kuenea kwake.

Hatua ambazo Tanzania imezianza sasa za kuchanja kwa hiari, ndivyo nchi zote duniani zilivyoanza lakini hali imeanza kubadilika baada ya baadhi ya huduma kuhitaji waliochanjwa pekee.

Agosti 10 mwaka huu, Kenya ilitoa siku 13 kwa watumishi wote wa umma nchini humo kuhakikisha wanapata chanjo dhidi ya Uviko-19 na kwamba watakaokiuka agizo hilo hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yao.

Baadhi ya kampuni nchini Uganda na Rwanda zilibandika matangazo yenye ujumbe kwa wafanyakazi wake kwamba hawataruhusiwa kufika kazini mpaka wawe wamechanja chanjo hiyo.

Nchini Marekani, Rais Joe Biden ameamuru wafanyakazi milioni mbili wa Serikali kuu kuonyesha uthibitisho wa chanjo au wafanyiwe vipimo vya lazima na kuvaa barakoa.

Kampuni nyingi kubwa ikiwemo Facebook na Google zimeweka wazi kuwa zitahitaji wafanyakazi kupewa chanjo wakati ofisi zitakapofunguliwa miezi michache ijayo kama ilivyo nchini Uzbekistan ambako chanjo ya hiari sasa imekuwa lazima kwa watoa huduma za jamii.

Agosti mwaka huu, Bunge la Ulaya na nchi wanachama walikubaliana kutoa cheti cha Uviko-19 ambacho kitatoa nafasi ya usafiri kote barani Ulaya katika kipindi cha utalii cha majira ya joto.

Wafanyakazi waachishwa kazi
Agosti 7 mwaka huu Shirika la habari nchini Marekani CNN liliwafuta kazi wafanyakazi watatu baada ya kwenda ofisini bila kupata chanjo hiyo.

Hata hivyo huo ni moja wapo ya mifano ya kwanza ya wamiliki wa kampuni za Marekani kuchukua hatua kama hiyo kukiuka mwongozo wa chanjo.

Mkuu wa CNN, Jeff Zucker alisema chanjo ni lazima kwa mtu yeyote anayeripoti nje ya ofisi, anayefanya kazi na wafanyakazi wengine wowote au kuingia ofisini.

Mashirika makubwa ya ndege, Delta na Shirika la Ndege la United yanahitaji wafanyakazi wapya kuonyesha uthibitisho wa chanjo.

Juni mwaka huu, Shirika la Ndege la Cathay Pacific la Hong Kong lilitoa sharti kwa kila mfanyakazi wake kupata chanjo hiyo, likienda mbali zaidi na kuagiza asiyetaka kuchanja aache kazi.

Mwananchi
 
Mimi Bado hamnipati asee borea mngekaa kimya baada ya kusema hiari ningeweza kuwafikiria ila hayo mambo ya kuanza kusema itakuwa lazima na me ndo naongeza mbio kuzikimbia hizo chanjo
 
Tatizo la umasishaji halipo kwa Tawala la Mikoa wala Serikali za mitaa, tatizo lipo Wizarani.

Ili mchakato uwe mwepesi uajibikaji kwa Viongozi ambao mwanzoni waliipinga chanjo ufanyike, sio dhambi kwa wao kujiuzuru ili ije nguvu mpya kasi mpya na hali mpya ya watu kuanza kuamini umuhimu wa chanjo.
 
Wengine bado wanaishi kwenye maono ya Hayati JPM na kuwaaminisha ni ngumu, wengine pia wanashindwa kuwaelewa viongozi wao kimsimamo
 
Back
Top Bottom