Rais wa Brazil aondolewa madarakani na Bunge kwa kuhusishwa na Rushwa

helu

Member
Feb 28, 2015
86
124
Baraza la Seneti nchini Brazil limeidhinisha kura ya kumfungulia mashitaka rais Dilma Roussef ambapo sasa amemuachia madaraka makamu wake ili mchakato wa kushitakiwa uendelee.

Hayo yamekuja saa chache tu baada ya baraza la seneti nchini Brazil kupiga kura 55 dhidi ya 22 jana Alhamis kumshitaki rais Dilma Rousseff, na kumuweka makamu wake wa rais Michel Temer madarakani katika mchakato ambao uliendelea usiku kucha wa kuamkia jana alhamis.

Kaimu Rais wa Brazili Michel Temer amewataka raia wa nchi hiyo kuungana kuiondoa nchi hiyo katika matatizo makubwa yanayoikabili.

Katika hotuba yake ya kwanza, toka alipochukua nafasi ya aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Dilma Roussef, (ambaye amesimamishwa katika nafasi yake kwa tuhuma za kutumia madaraka vibaya), Temer amesema Brazil ni lazima ijenge tena sifa yake nje ya nchi hiyo kuweza kuvutia tena wawekezaji na uchumi wa nchi hiyo kukua tena.

Jitihada za rais huyo kuepukana na kikaango cha kuondolewa madarakani , zilififia siku ya jumatano baada mahakama kukataa ombi la mwanasheria mkuu la kubatilisha mchakato huo.

"Neno langu la kwanza kwa Wabrazil ni neno uaminifu. Uaminifu katika maadili ambayo yanajenga hadhi ya mtu. Katika uimara wa demokrasia. Uaminifu katika kuufufua uchumi wa nchi yetu." Temer amesema.

Pia ameahidi kuunga mkono uchunguzi mpana zaidi kuhusiana na rushwa na ufisadi katika kampuni la taifa la mafuta ambao tayari unawagusa wanasiasa maarufu kutoka vyama mbali mbali.

Mamia ya waandamanaji waliingia mitaani katika mji wa Sao Paulo baada ya kura ya Seneti ya kumvua madaraka yake rais Dilma Rousseff hatua inayosafisha njia rais huyo kushitakiwa kwa kuvunja sheria za bajeti.

Baadhi ya watu waliokuwa wakishangiria mjini Sao Paulo na miji mingine walijifunika bendera ya Brazil ya rangi ya kijani, njano na buluu, wakati baadhi ya wafuasia wa Rousseff wakiandamana pia.

Rais Dilma Rousseff , aliondoka Ikulu ya Planalto katika mji mkuu Brasilia huku maelfu ya wanaomuunga mkono wakijikusanya kumuaga.
 
Back
Top Bottom