Patriot
JF-Expert Member
- Feb 11, 2008
- 5,703
- 4,697
Miaka mingi tumelalamikia tabia ya wanasiasa kutaka kuwa ni viumbe muhimu sana kuliko wengine ktk nchi hii, lakini hatukuwahi kupata mkombozi wa tatizo hili. Wanasiasa walidai malipo mazuri, spika Sitta akapandisha kipato hadi kuwaambia "mbunge siyo mtu wa kuishi kwa shida". Wabunge walidai kupigiwa saluti, ikashindikana! Walidai wapewe pesa za jimbo ili wagawe wanapotembelea wananchi, wakapewa lakini ikawa siyo ya kwao mfukoni. wabunge wanajipangia marupurupu. Wana mfuko wao wa matibabu tofauti na wananchi wengine. Waziri mmoja aliwahi hata kukaa ndani ya ATM machine muda mrefu akipiga simu wakati wananchi wakisubili nje bila kujali.
Kwa ujumla wanasiasa wamepewa nguvu kiasi kwamba sasa hata barabarani hawafuati sheria za usalama. Spidi mtindo mmoja! Ni kama hawaamini kwamba ni binadamu wa kawaida.
Kwa haya yanayotokea, ni wazi wameanza kuhisi ubinadamu wao. Wao ni wenzetu. Rais ongeza nguvu ili wajitambue kwamba tuko pamoja. Lakini ni kazi kubwa. Wengi wamelemaa na baadhi ya wananchi wanadhani ndivyo inavyotakiwa. Si unaona mtu anafukuzwa uwaziri anagomba utadhani alipewa na mazazi kama jina lake? Tusaidie kuondoa nyodo hizi.